Makatibu Wakuu wakutana Dar es Salaam kujadili changamoto za Muungano

Katibu Mkuu Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) Bw. Thabit Idarous Faina (kulia) akiongoza Kikao cha Sekretarieti ya Kamati ya Pamoja SMT na SMZ ya kushughulikia masuala ya Muungano kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Vuga, Zanzibar leo tarehe 16/08/2021. Katikati ni Mwenyekiti Mwenza wa Kikao hicho Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (SMZ) Bi. Mary Ngelela Maganga. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Muungano Bi. Cesilia Nkwamu.
Picha ikionyesha wajumbe wakifuatilia mjadala katika Kikao cha Sekretarieti ya Kamati ya Pamoja SMT na SMZ ya kushughulikia masuala ya Muungano kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Vuga, Zanzibar leo tarehe 16/08/2021. Kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (SMZ) Bi. Mary Ngelela Maganga na Kushoto ni Bi. Siajabu Suleiman Pandu, Mkurugenzi wa Uratibu wa Shughuli za Serikali katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Emmanuel Tutuba na Bw. Christopher Kadio Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) wakifuatilia kikao cha pamoja na Makatibu Wakuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kilichofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu – Dar es Salaam leo tarehe 10/08/2021.

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *