Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akizungumza na Balozi wa Misri nchini Tanzania Mhe. Mohamed Gaber Abulwafa alipofika Ofisi ya Makamu wa Rais Dar es Salaam leo Agosti 18, 2022 katika kikao kilichozungumzuia masuala mbalimbali yakiwemo maandalizi ya Mkutano wa 27 wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi unaotarajiwa kufanyika nchini Misri Novemba mwaka huu.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akizungumza na Balozi wa Misri nchini Tanzania Mhe. Mohamed Gaber Abulwafa alipofika Ofisi ya Makamu wa Rais Dar es Salaam kufanya mazungumzo leo Agosti 18, 2022 kuzungumzuia masuala mbalimbali yakiwemo maandalizi ya Mkutano wa 27 wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi unaotarajiwa kufanyika nchini Misri Novemba mwaka huu. Kushoto ni Mkurugenzi wa Mazingira Dkt. Andrew Komba.
Balozi wa Misri nchini Tanzania Mhe. Mohamed Gaber Abulwafa akimkabidhi zawadi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo mara baada ya kufanya mazungumzo katika Ofisi ya Makamu wa Rais jijini Dar es Salaam leo Agosti 18, 2022 kuhusu maandalizi ya Mkutano wa 27 wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi unaotarajiwa kufanyika nchini Misri Novemba mwaka huu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Misri nchini Tanzania Mhe. Mohamed Gaber Abulwafa mara baada ya kumalizi kikao ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo Agosti 18, 2022 kuzungumzuia masuala mbalimbali yakiwemo maandalizi ya Mkutano wa 27 wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi unaotarajiwa kufanyika nchini Misri Novemba mwaka huu.

==================================================================

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Selemani Jafo amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Misri nchini Tanzania Mohamed Gaber Abulwafa katika Ofisi ya Makamu wa Rais jijini Dar es Salaam juzi.

Pamoja na mambo mbalimbali kikao hicho kimezungumzuia maandalizi ya Mkutano wa 27 wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP27) unaotarajiwa kufanyika nchini Misri Novemba mwaka huu.

Dkt. Jafo alisema hii ni heshima kubwa kwa Bara la Afrika kushiriki katika mkutano huo na kwamba ushiriki wa Tanzania utatoa fursa katika kutangaza namna inavyoshirikiana na wadau katika hifadhi ya mazingira.

“Nikiri wazi ushiriki wetu kule Misri utakuwa mzuri na mpana na tayari tumeanza kufanya maandalizi ya ushiriki tukiwa taasisi zetu na wadau wegine ambapo tunatarajia kuonesha kazi zetu kupitia mkutano huo,” alisema.

Aliongeza kuwa Tanzania pamoja na nchi nyingine barani Afrika zimekuwa zikipata changamoto za uharibifu wa mazingira na mkutano huo utazikutanisha nchi hizo nan chi zinazoendelea kujadili namna ya tatumia jukwaa hilo

Hivyo alisema Tanzania itaendelea kusukuma ajenda ya kuzitaka nchi nchi zinazoendelea kutoa fedha barani Afrija kwa ajili ya kupambana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Kwa upande wake Balozi Abulwafa alisema kuwa nchi yake inatarajia Tanzania itanufaika na COP27 kwa vile ni mojawapo ya nchi zinazoathiriwa na mabadiliko ya tabianchi.

Hata hivyo, alipongeza jitihada zinazofanywa na Tanzania chini ya Rais Samia Suluhu Hassa ambaye ameshiriki kikamilifu katika mikutano mbalimbali yenye ajenda ya kupambana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Itakumbukwa kuwa Tanzania imeungana na Jumuiya ya kimataifa kupitisha na kutekeleza azimio la kuhifadhi misitu duniani na wito umetolewa kwa wakuu wa mikoa, wilaya na halmashauri zote nchini kutekeleza maagizo ya kupanda miti 1,500,000 kila mwaka ili kuuunga mkono na kufanikisha jitihada za kuhimili mabadiliko ya tabianchi.

Aidha, miradi ya Kimkakati ya Treni ya Umeme (SGR), Mradi wa Umeme wa Maji wa Mwalimu Nyerere na Mradi wa Mabasi yaendayo kasi (BRT) imekuwa ni miradi ya mfano kimataifa katika kukabiliana na athari hizo.

Vilevile, Waziri Jafo alisisitiza kuwa sekta binafsi ishirikiane na Serikali na wadau wengine katika kutekeleza maazimio ya Mkutano wa COP26 na mikakati ya Serikali ya kukabiliana na kuhimili mabadiliko ya tabianchi.

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *