Katika ziara hiyo Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga (kulia) akiongoza Menejimenti ya Ofisi kukagua jengo linalojengwa katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma, ziara iliyofanyika leo tarehe 03 Oktoba, 2023. Wa pili kulia ni Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Bw. Abdallah Hassan Mitawi.

Katika ziara hiyo Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga (katikati) akiangalia maendeleo ya ujenzi wa jengo la Ofisi hiyo unaoendelea katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma, ziara iliyofanyika leo tarehe 03 Oktoba, 2023. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Bw. Abdallah Hassan Mitawi.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga (kulia) akiongoza Menejimenti ya Ofisi kukagua jengo linalojengwa katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma, ziara iliyofanyika leo tarehe 03 Oktoba, 2023.

=====================================================================

Menejimenti ya Ofisi ya Makamu wa Rais imefanya ziara ya kukagua ujenzi wa jengo la Ofisi hiyo unaoendelea katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma leo tarehe 03 Oktoba, 2023.

Ujenzi wa jengo hilo lenye thamani ya shilingi 18.8 unatekelezwa na Kampuni ya ujenzi ya SUMA JKT kwa kushirikiana na Msimamizi Elekezi ambaye ni Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).

Katika ziara hiyo Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga akiongoza ujumbe wa menejimenti hiyo amemtaka mkandarasi kuongeza kasi ya ujenzi wa jengo hilo ili likamilike Kwa wakati

Kutokana na changamoto ya kupungua kasi ya ujenzi huo amemtaka mkandarasi kupitia upya mpango kazi kubainisha ni lini ujenzi huo utakuwa umekamilika ndani ya kipindi kifupi.

“Tunatambua mpo nyuma ya muda katika shughuli za ujenzi lakini bado tunahitaji jengo hili likamilike haraka ili watumishi waweze kuingia na kutekeleza majukumu yao,“ amesisitiza Bi. Maganga.

Mkataba wa ujenzi wa jengo hilo ulifanyika Dodoma Oktoba 13, 2021 huku ukitarajiwa kukamilika Novemba 2023.

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *