Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango na Mkewe Mama Mbonimpaye Mpango leo tarehe 04 Septemba 2022 wakizungumza na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Ali Hassan Mwinyi pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Hussein Ali Mwinyi mara baada ya kuhani msiba Chukwani Mjini Zanzibar kufuatia kifo cha Hassan Ali Mwinyi ambaye ni mtoto wa Rais mstaafu Mwinyi kilichotokea tarehe 31 Agosti 2022.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akimpa pole Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Ali Hassan Mwinyi kufuatia kifo cha mtoto wake Hassan Ali Mwinyi kilichotokea tarehe 31 Agosti 2022 mara baada ya kufika kuhani msiba huo nyumbani kwa marehemu Chukwani mjini Zanzibar leo tarehe 04 Septemba 2022.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akimpa pole Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi kufuatia kifo cha kaka yake Hassan Ali Mwinyi kilichotokea tarehe 31 Agosti 2022 mara baada ya kufika kuhani msiba huo nyumbani kwa marehemu Chukwani mjini Zanzibar leo tarehe 04 Septemba 2022.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akimpa pole Mama Siti Mwinyi kufuatia kifo cha mtoto wake Hassan Ali Mwinyi kilichotokea tarehe 31 Agosti 2022 mara alipofika kuhani msiba huo nyumbani kwa marehemu Chukwani mjini Zanzibar leo tarehe 04 Septemba 2022.

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *