Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Philip Mpango akisalimiana na Waziri wa Mipango na Maendeleo wa Ivory Coast Mheshimiwa Kaba Nialé mara alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Félix Houphouët Boigny Abidjan nchini Ivory Coast leo tarehe 31 Oktoba 2022. (Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Nigeria ambaye anaiwakilisha pia Tanzania nchini Ivory Coast Dkt.Benson Bana).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Philip Mpango akipokelewa na baadhi ya watanzania waishio nchini Ivory Coast mara baada ya kuwasili Abidjan leo tarehe 31 Oktoba 2022.

===================================================================

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMhe. Dkt. Philip Mpango leo tarehe 31 Oktoba 2022 amewasili Abidjan nchini Ivory Coast ambapo atamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika Jukwaa la Uwekezaji Barani Afrika litakalofanyika tarehe 02-04 Novemba 2022.

Makamu wa Rais anatarajia kuongoza mazungumzo baina ya Tanzania na wawekezaji mbalimbali kuhusu uwekezaji katika miradi ya kimkakati nchini Tanzania katika sekta ya Kilimo cha Umwagiliaji, Usafirishaji na Uchukuzi.

Jukwaa la Uwekezaji Barani Afrika linaratibiwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kwa kushirikiana na waanzilishi wa Jukwaa hilo na linalenga kuwakutanisha Wawekezaji, Sekta Binafsi na Sekta ya Umma ili kuweka mikakati ya kufadhili miradi endelevu.

Jukwaa hilo linashirikisha Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika, Wakuu wa taasisi na mashirika ya kimataifa pamoja na wafanyabiashara.

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *