Naibu Waziri Khamis ateta na Mjumbe wa Uingereza

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Khamis Hamza Khamis (kulia) akisalimiana na Bi. Janet Rogan mjumbe kutoka Serikali ya Uingereza katika Mkutano wa 27 wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi unaoendelea Sharm El-Sheikh, Misri. Katika kikao hicho Tanzania na Uingereza zimekubaliana kuendelea kuimarisha ushirikiano uliopo baina ya nchi mbili.

Mjumbe kutoka Serikali ya Uingereza Bi. Janet Rogan akifafanua jambo kwa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis na ujumbe wake katika kikao cha ushirikiano kilichofanyika katika Mkutano wa 27 wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi unaoendelea Sharm El-Sheikh, Misri leo tarehe 16 Novemba 2022.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Khamis Hamza Khamis (kulia) akimkaribisha Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Bi. Patricia Scotland katika banda la Tanzania kwenye Mkutano wa 27 wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi unaoendelea Sharm El-Sheikh, Misri. Bi. Scotland ameipongeza Tanzania kwa jitihada za kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi.

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *