Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akimkabidhi Waziri wa Mazingira, Kilimo na Mifugo wa Burundi Prof. Sanctus Niragira, uenyekiti wa Mkutano wa 10 wa Mawaziri waliopo katika Mktaba wa Kikanda wa Usimamizi Endelevu wa Ukanda wa Ziwa Tanganyika uliofanyika jana jijini Bujumbura nchini Burundi, ambapo Tanzania imemaliza muda wake.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akizungumza wakati wa Mkutano wa 10 wa Mawaziri waliopo katika Mktaba wa Kikanda wa Usimamizi Endelevu wa Ukanda wa Ziwa Tanganyika uliofanyika jana jijini Bujumbura nchini Burundi ambapo Tanzania ilikabidhi kijiti cha uenyekiti kwa mwanachama Burundi baada ya kumaliza muda wa uongozi wa mwaka mmoja.
Waziri wa Mazingira, Kilimo na Mifugo wa Burundi Prof. Sanctus Niragira ambaye ni Mwenyekiti mpya wa Mkutano wa wa Mawaziri waliopo katika Mktaba wa Kikanda wa Usimamizi Endelevu wa Ukanda wa Ziwa Tanganyika akiuzugumza mara baada ya kukabidhiwa kijiti na Tanzania kupitia kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo katika Mkutano wa 10 wa Mawaziri hao uliofanyika jana jijini Bujumbura nchini Burundi, ambapo Tanzania imemaliza muda wake wa uenyekiti.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Dkt. Switbert Mkama akishiriki Mkutano wa 10 wa Mawaziri waliopo katika Mktaba wa Kikanda wa Usimamizi Endelevu wa Ukanda wa Ziwa Tanganyika uliofanyika jana Bujumbura nchini Burundi ambapo Tanzania ilikabidhi kijiji cha uenyekiti kwa Burundi.
Mkurugenzi wa Mazingira Dkt. Andrew Komba akishiriki Mkutano wa 10 wa Mawaziri waliopo katika Mktaba wa Kikanda wa Usimamizi Endelevu wa Ukanda wa Ziwa Tanganyika uliofanyika jana Bujumbura nchini Burundi ambapo Tanzania ilikabidhi kijiji cha uenyekiti kwa Burundi.
Afisa Mazingira Mkuu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Deogratius Nyangu akishiriki Mkutano wa 10 wa Mawaziri waliopo katika Mktaba wa Kikanda wa Usimamizi Endelevu wa Ukanda wa Ziwa Tanganyika uliofanyika jana Bujumbura nchini Burundi ambapo Tanzania ilikabidhi kijiji cha uenyekiti kwa Burundi.
====================================================================

SERIKALI ya Tanzania imeikabidhi Burundi kiti cha uenyekiti wa Mawaziri waliopo katika Mkataba wa Kikanda wa Usimamizi Endelevu wa Ukanda wa Ziwa Tanganyika na kusisitiza Kiswahili kitumike kama lugha kuu ya mawasiliano katika mikutano yote itakayofanyika.

Hayo yamefanyika wakati wa Mkutano wa 10 wa Mawaziri hao uliofanyika jana jijini Bujumbura nchini Burundi baada ya Tanzania kumaliza muda wa uenyekiti uliodumu kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Akizungumza wakati wa mkutano huo Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo alisema Tanzania inashiriki katika shughuli zote zinazolenga kuhakikisha usimamizi endelevu wa rasilimali za ziwa hilo.

Pia, alisema Tanzania imedhamiria kushirikiana na nchi wanachama ambazo ni Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Zambia katika utekelezaji wa programu za kikanda zinazolenga kulinda rasilimali za pamoja za Ziwa Tanganyika na kuboresha maisha ya watu katika bonde hilo.

Dkt. Jafo alisema Ziwa Tanganyika ni rasilimali muhimu kwa wananchi takriban milioni 10 wa ukanda huo wanaolizunguka hivyo zinahitajika juhudi za pamoja katika kulilinda.

“Waheshimiwa mawaziri, mazingira tunayoishi yanabadilika haraka sana na shughuli za binadamu zinatumia maliasili za dunia kwa kasi ya kutisha na kuharibu mifumo ikolojia. Inakadiriwa kuwa zaidi ya viumbe 22,000 wako hatarini kutoweka ikiwa ni pamoja na baadhi ya viumbe katika Ziwa Tanganyika,” alisema.

Hivyo, alitoa wito kwa Mawaziri hao kutoka nchi wanachama kuungana kwa pamoja kujadili namna bora ya kulinda Ziwa Tanganyika kwa leo na kizazi kijacho huku akisisitiza umuhimu wa kuweka utaratibu wa muda mrefu wa ufadhili wa programu ya maendeleo ya Ukanda ya Ziwa Tanganyika.

Ujumbe ulioshiriki katika Mkutano huo uliwashirikisha pia Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Dkt. Switbert Makama, Mkurugenzi wa Mazingira Dkt. Andrew Komba, Afisa Mazingira Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Deogratius Nyangu na uwakilishi wa Wizara ya Fedha na Mipango pamoja ba Wizara ya Mifugo na Uvuvi.   

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *