Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis akizungumza na viongozi huo kufuatilia utekelezaji wa Mradi wa Kuhifadhi Ardhi katika Bonde la Ziwa Nyasa unaoratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis akiwasili katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma kwa ajili ya kikao na viongozi wa wilaya hiyo kufuatilia utekelezaji wa Mradi wa Kuhifadhi Ardhi katika Bonde la Ziwa Nyasa unaoratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais.

=================================================================

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis amewataka wachimbaji wa makaa ya mawe kuzingatia sheria kwa kufukia mashimo baada ya shughuli hiyo.

Ametoa kauli hiyo alipofanya kikao na uongozi wa Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma wakati wa ziara ya kufuatilia utekelezaji wa Mradi wa Kuhifadhi Ardhi katika Bonde la Ziwa Nyasa unaoratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais.

Kutokana na changamoto hiyo Mhe. Khamis amewataka viongozi kusimamia maelekezo yaliyotolewa na Serikali kuhakikisha wamiliki wa migodi hiyo pamoja na kuwa wanawekeza lakini wanapaswa kujali mazingira.  

Pia, amewataka wenye magari yanayobeba makaa ya mawe kuyafunika ili kuepusha vumbi linaloweza kusambaa na kusababisha madhara kiafya na mazingira kwa ujumla.

Amesema kuwa ni kweli Serikali inawathamini wawekezaji mbalimbali wakiwemo wa sekta ya madini lakini wanapaswa kufuata sheria ili kunusuru mazingira kwa maendeleo endelevu ya nchi.

Awali Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Aziza Mangosongo amesema bado kuna changamoto ya wananchi kufanya shughuli za kibinadamu kando ya mito na kusababisha uharibifu wa mazingira.

Pia, amesema baadhi ya wenye migodi hukata miti kwa matumizi yao wakidai kuwa leseni ya uchimbaji inawapa kibali cha kutumia kila kitu wanachokikuta katika eneo walilopewa kufanya uwekezaji huo, hali inasavavisha uharibifu wa mazingira.

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *