Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis amesema Serikali itaanza kujenga ukuta wa Ikulu ndogo ya Muungano, Pemba katika mwaka wa fedha 2024/25.

Amesema hayo bungeni Dodoma leo Januari 30, 2024 wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Wete Mhe. Omar Ali Omar aliyetaka kujua ni lini Serikali itaanza kujenga ukuta Ikulu ndogo ya Muungano Pemba.

Mhe. Khamis amesema kuwa tayari Serikali imeshaandaa mipango mahsusi ya kutekeleza ujenzi huo kwa kufanya tathmini ya kitaalkamu ya kina ikiwemo ujenzi wa ukuta.

Kuhusu mipango ya kufanya upembuzi yakinifu kabla ya kujenga ukuta, Naibu Waziri amesema ni muhimu kufanya tathmini kujua gharama halisi ili kutekeleza kazi hiyo.

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *