Hospitali ya Benjamin Mkapa yahimizwa kuendelea kutunza mazingira

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga akiongoza Menejimenti ya Ofisi hiyo katika kikao na Uongozi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa kilichofanyika katika Mji wa Serikali, Mtumba jijini Dodoma ambapo amewapongeza kwa utunzaji wa mazingira. 

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa Dkt Alphonce Chandika mara baada ya kikao kati ya Menejimenti ya Ofisi hiyo na Uongozi wa Hospitali hiyo kilichofanyika katika Mji wa Serikali, Mtumba jijini Dodoma ambapo amewapongeza kwa utunzaji wa mazingira.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Ofisi hiyo na Uongozi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa mara baada ya kikao kilichofanyika katika Mji wa Serikali, Mtumba jijini Dodoma ambapo amewapongeza kwa utunzaji wa mazingira.

============================================================================

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga ametoa wito kwa Uongozi Hospitali ya Benjamin Mkapa kuendelea kushiriki katika utunzaji wa mazingira ikiwemo kupanda miti na usafi wa mazingira.

Bi. Maganga ametoa wito huo wakati Menejimenti ya Ofisi ya Makamu wa Rais ilipokutana na Uongozi wa Hospitali hiyo katika kikao kilichofanyika katika Mji wa Serikali jijini Dodoma.

Amehimiza shughuli za upandaji wa miti na usafi wa mazingira hususan katika kutenganisha taka zinazofanyika katika hopsitali hiyo ziendelee kuwa za mfano kwa taasisi zingine.

Ameupongeza na kuushukuru uongozi wa hospitali hiyo inayohudumia Mkoa wa Dodoma na mikoa ya jirani kwa usimamizi mzuri ambao umechangia utoaji wa huduma bora za afya kwa wananchi mbalimbali.

Halikadhalika, ameuomba uongozi wa hospitali hiyo kuandaa mafunzo kwa watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais kuhusu masuala mbalimbali ya afya yakiwemo afya ya akili na umuhimu wa uchangiaji wa damu.


Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dkt Alphonce Chandika ameishukuru Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kuwapa ushirikiano katika shughuli za utunzaji wa mazingira.


Pia, Dkt. Chandika ameomba Ofisi hiyo kutoa mtaalamu wa mazingira atakayekuwa na jukumu la kushirikiana nao katika utoaji wa elimu ya masuala ya mazingira.

Ameongeza kuwa wako tayari kutoa elimu kwa watumishi katika eneo hilo pindi watakapohitajika huku wakiendelea kutoa huduma bora za afya.

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *