Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akifungua Maonesho ya Biashara Miaka 60 ya Muungano katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo Aprili 19, 2024.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis akitoa salamu wakati wa Maonesho ya Biashara Miaka 60 ya Muungano katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo Aprili 19, 2024 ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Cyprian Luhemeja akitoa neno la ukaribisho wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Biashara Miaka 60 ya Muungano katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo Aprili 19, 2024 ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar e s Salaam Edward Mpogolo akizungumza Wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Biashara Miaka 60 ya Muungano katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo Aprili 19, 2024 ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla.

Washiriki mbalimbali wakifuatilia ufunguzi wa Maonesho ya Biashara Miaka 60 ya Muungano katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo Aprili 19, 2024 ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla.

============================================================================

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Hemed Suleiman Abdulla ameipongeza Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kutoa elimu kuhusu masuala ya Muungano.

Ametoa pongezi hizo wakati akizindua maonesho ya Biashara ya Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar hafla iliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar- es- Salaam ikiwa ni katika shamra shamra za sherehe za miaka 60 ya Muungano.

Amesema kuwa banda la maonesho la Ofisi ya Makamu wa Rais lililopo katika viwanja hivyo limesheheni vitabu na maandiko mbalimbali yanayohusu Muungano adhimu. 

Mhe. Hemed ambaye alitembelea banda hilo mara alipowasili, ametoa wito kwa wananchi wote kulitembea na kupata elimu kutoka kwa wataalamu wa Ofisi hiyo. 

Aidha, amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) itaendelea kuuenzi kuulinda Muungano huku akiwataka wananchi kushiriki katika kuujua Muungano. 

Halikadhalika, Makamu wa Pili wa Rais amesema kuwa uwepo wa Muungano umechangia kuimarika kwa huduma za kijamii kwa pande zote mbili za Muungano kama vile Sekta ya Maji safi na salama, Afya, elimu, ustawi na maendeleo ya jamii, makazi na usafiri.

Amesema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar umechangia kwa kiasi kikubwa kuimarika kwa udugu wa damu na urafiki ambao umepunguza migawanyiko ya kijamii na kuondoa hisia za ukabila na ubaguzi miongoni mwa wananchi. 

Mhe. Hemed ameeleza kuwa ustawi wa wananchi umeimarika na kukua kwa uchumi kulikotoa fursa kwa wafanyabiashara wakubwa na wadogo kuwekeza katika pande zote mbili za Muungano katika sekta ya Viwanda, Hoteli na kilimo cha biashara jambo ambalo linachangia kuongeza ajira kwa wananchi.

Logo
OFISI YA MAKAMU WA RAIS
WASILIANA NASI

Katibu Mkuu 

Ofisi ya Makamu wa Rais, 

Mji wa Serikali,

Eneo la Mtumba,

Jengo la Makamu wa Rais,

S.L.P. 2502,

40406DODOMA.

Barua pepe:  ps@vpo.go.tz

Simu:  (255) (26) 232 9006

Nukushi:  + (255) 026 2329007/2963150

VIVUTIO VYA NCHI 

Mlima Kilimanjaro

Hifadhi za Selous

Mji Mkongwe

Hifadhi ya Serengeti

Mapango ya Amboni

Hifadhi ya Ngorongoro

TOVUTI MASHUHURI 

National Carbon Monitoring Centre

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira

Wakala wa Misitu Tanzania

Taasisi ya Utafiti wa Wanyapori

Tanzania Environmental Experts Association

Environmental Information Network – TanzaniaRamani ya TovutiSera ya FaraghaVigezo na MashartiHakimilikiKanusho

Imesanifiwa, Imetengenezwa na Inahifadhiwa na Mamlaka ya serikali Mtandao Taarifa zinasimamiwa na VPO

© 2020 – 2024 Ofisi ya Makamu wa Rais. Haki zote zimehifadhiwa

https://www.ega.go.tz/special-announcement

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *