Watoto kutoka kituo cha kulea watoto yatima cha Mazizini kilichopo Wilaya ya Magharibi ‘B’ Mkoa wa Mjini Magharibi wakishiriki Futari iliyoandaliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango iliyofanyika katika Kituo cha Wazee Sebleni Wilaya ya Mjini Unguja, Zanzibar tarehe 05 Aprili 2024.

Wazee mbalimbali kutoka katika Kituo cha Wazee Sebleni kilichopo Wilaya ya Mjini Unguja, Zanzibar wakishiriki Futari iliyoandaliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Philip Mpango kwaajili ya Makundi Maalum tarehe 05 Aprili 2024.

Viongozi na watumishi mbalimbali kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira wakishiriki futari pamoja na Wazee kutoka katika Kituo cha Wazee Sebleni kilichopo Wilaya ya Mjini na Watoto kutoka kituo cha kulea watoto yatima cha Mazizini kilichopo Wilaya ya Magharibi ‘B’ Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Zanzibar iliyoandaliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango kwaajili ya Makundi Maalum tarehe 05 Aprili 2024.

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *