Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango na Mwenza wake Mama Mbonimpaye Mpango wameshiriki katika Ibada Maalum ya kumbukizi ya Miaka 40 ya kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Edward Moringe Sokoine iliyofanyika katika Kijiji cha Enguiki Wilaya ya Monduli mkoani Arusha tarehe 12 Aprili 2024.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Edward Moringe Sokoine mara baada ya Ibada Maalum ya kumbukizi ya Miaka 40 ya kifo cha Hayati Edward Sokoine iliyofanyika katika Kijiji cha Enguiki Wilaya ya Monduli mkoani Arusha tarehe 12 Aprili 2024.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwaaga wajane wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Edward Moringe Sokoine (wenye nguo nyeupe) Nekiteto Sokoine (kulia) na Napono Sokoine (kushoto) mara baada ya Ibada Maalum ya kumbukizi ya Miaka 40 ya kifo cha Edward Sokoine iliyofanyika katika Kijiji cha Enguiki Wilaya ya Monduli mkoani Arusha tarehe 12 Aprili 2024.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwaaga wananchi wa Monduli Juu mara baada ya kushiriki Ibada Maalum ya kumbukizi ya Miaka 40 ya kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Edward Moringe Sokoine iliyofanyika katika Kijiji cha Enguiki Wilaya ya Monduli mkoani Arusha tarehe 12 Aprili 2024.

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *