Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, akikagua banda la Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika Viwanja vya Maonesho ya Biashara Nyamanzi Mkoa wa Mjini Magharibi leo Aprili 14, 2024.

Uzinduzi huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo, Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Cyprian Luhemeja na Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Bw. Abdallah Hassan Mitawi.

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *