Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akinunua vitabu katika maduka mbalimbali jijini Dar es salaam  ikiwemo Duka la Mkuki na Nyota pamoja na Duka la Pauline’s Bookshop kwa lengo la kujisomea vitabu hivyo vilivyoandikwa na waandishi wa ndani na nje ya nchi. Makamu wa Rais hutumia muda wa mapumziko katika kujisomea vitabu kwa lengo la kuongeza maarifa katika sekta mbalimbali za uchumi, utawala, dini, siasa, kilimo na ufugaji. 

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *