Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu Rasmi ya Ofisi ya Makamu wa Rais

Balozi Luvanda afanya mazungumzo na UNOPS
Mar 25, 2026
Balozi Luvanda afanya mazungumzo na UNOPS
Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe. Balozi Baraka Luvanda akifanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Huduma za Miradi (UNOPS) Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini Bw. Rainer Frauenfeld jijini Dodoma Machi 25, 2026.
Na robert Hokororo

==================================================================================================================

Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe. Balozi Baraka Luvanda amekutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Huduma za Miradi (UNOPS).

Kikao hicho kimefanyika Machi 26,2026 jijini Dodoma kikiwa na lengo la kuongeza ushirikiano katika masuala ya Hifadhi za Mazingira na Jitihada za kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi.

Balozi Luvanda kwa niaba ya Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt Richard Muyungi amelipongeza Shirika hilo kwa kuendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika Miradi mbalimbali ya hifadhi ya mazingira ikiwemo mradi wa Hifadhi na Bioanuai unaotekelezwa katika Bonde la Ziwa Tanganyika kupitia Mkataba wa Usimamizi Endelevu wa Ziwa Tanganyika ambao Tanzania ni Mwanachama.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa UNOPS Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini Bw. Rainer Frauenfeld ameishukuru Tanzania kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kuendelea kushirikiana na UNOPS akikisitiza kuwa Shirika hilo lipo tayari kushirikiana na Serikali.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi