

Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Richard Muyungi akipata maelezo mbalimbali kuhusu sekta ya madini alipotembelea banda la Tume ya Madini katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) leo Julai 11, 2026.
================================================================================================================
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Richard Muyungi ametembelea banda la Tume ya Madini katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) leo Julai 11, 2026.
Akizungumza mara baada ya kutembelea banda hilo aliipongeza Tume ya Madini kwa utoaji wa elimu kwa umma kuhusu rasilimali za madini na fursa zilizopo katika sekta hiyo.
Pia, Dkt. Muyungi alisema kuwa sekta hiyo hiyo ina mchango mkubwa katika kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu umuhimu wa rasilimali za madini, fursa za uwekezaji na nafasi ya sekta ya madini katika kukuza uchumi na maendeleo endelevu ya taifa.