=====================================================================================
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango ameongoza Kikao cha Kamati ya Pamoja ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SJMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) ya kushughulikia Masuala ya Muungano kilichofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe 04 Aprili 2025.
Katika Kikao masuala mbalimbali yanayohusu Muungano yamejadiliwa kwa lengo la kutatua hoja mbalimbali na kuimarisha zaidi Muungano.
Kikao hicho kimehudhuriwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, Naibu Waziri Mkuu Mhe. Dotto Biteko, Waziri Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhandisi Hamad Masauni na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili ya Rais (Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi) Mhe. Hamza Hassan Juma.
Wengine ni Mawaziri na Manaibu Mawaziri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Katibu Mkuu Kiongozi Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Balozi Dkt. Moses Kusiluka , Katibu Mkuu Kiongozi Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhandisi Zena Said, Makatibu Wakuu, Wakuu wa Taasisi pamoja na Wataalamu mbalimbali.