Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu Rasmi ya Ofisi ya Makamu wa Rais

Balozi Luvanda ahimiza umuhimu wa mazoezi kwa watumishi
Mar 14, 2026
Balozi Luvanda ahimiza umuhimu wa mazoezi kwa watumishi
Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe. Balozi Baraka Luvanda (wa pili kulia) akijumuika na watumishi wa ofisi hiyo katika bonanza la mazoezi ya pamoja lililolenga kujenga afya na kuimarisha utimamu wa miili lililofanyika Machi 14, 2026 jijini Dodoma.
Na Robert Hokororo

Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe. Balozi Baraka Luvanda (kushoto) akijumuika na watumishi wa ofisi hiyo katika bonanza la mazoezi ya pamoja lililolenga kujenga afya na kuimarisha utimamu wa miili lililofanyika Machi 14, 2026 jijini Dodoma.

Watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais wakishiriki bonanza la mazoezi ya pamoja lililolenga kujenga afya na kuimarisha utimamu wa miili lililofanyika Machi 14, 2026 jijini Dodoma.

==================================================================================================================

Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe. Balozi Baraka Luvanda amewahimiza watumishi wa ofisi hiyo kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi ili kuimarisha afya na kuongeza ufanisi kazini.

Mhe. Luvanda ametoa rai hiyo Machi 14 2026 Jijini Dodoma wakati alipojumuika na watumishi wa ofisi hiyo katika bonanza la mazoezi ya pamoja iliyolenga kujenga afya na kuimarisha utimamu wa miili.

Amesema mazoezi jambo muhimu linalopaswa kuzingatiwa na watumishi wote kwani linasaidia kuimarisha afya na mapambano dhidi ya maradhi yasiyoambukiza na kusisitiza umuhimu wa kupewa kipaumbele katika maisha ya kila siku.

“Mazoezi ni afya na pia ni daktari…ukijenga utamaduni wa kufanya mara kwa mara utakusaidia wewe binafsi hivyo ni suala la umuhimu linalopaswa kuzingatiwa na kupewa msukumo” amesema Mhe. Luvanda.

Aidha Balozi Luvanda amesisitiza umuhimu wa watumishi wote wa Ofisi hiyo kujitokeza katika viwanja vya mazoezi kila mwishoni mwa wiki kwani kutasaidia kujenga morali na hamasa ya kuhusu umuhimu wa bonanza hilo ambalo ni muhimu kwa afya.

“Idadi tuliojitokeza bado ni ndogo ikilinganishwa na idadi halisi ya watumishi tuliopo, nawasihi wenzetu wengine waendelee kujitokeza ili kulipa uzito na umuhimu wa kipekee bonanza hili’ amesema Mhe. Luvanda.

Katika bonanza hilo lilihusisha michezo ya mazoezi ya viungo, mpira wa pete, mpira wa miguu pamoja na riadha.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi