Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu Rasmi ya Ofisi ya Makamu wa Rais

CHANETA, CHANEZA zajengewa uwezo kuhusu Muungano
Oct 01, 2026
CHANETA, CHANEZA zajengewa uwezo kuhusu Muungano
Mkurugenzi wa Muungano Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Juma Mohamed Salum akifafanua jambo wakati wa kikao kazi cha kuwajengea uwezo wasanii, Viongozi wa Vyama vya Mpira wa pete - Netboli Tanzania Bara na Zanzibar (CHANETA & CHANEZA) wakati wa kikao kilichofanyika leo Oktoba 01, 2026 katika Ofisi ndogo ya Makamu wa Rais, Luthuli Jijini Dar es Salaam.
Na Robert Hokororo

Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Sarah Kibonde akifafanua jambo wakati wa kikao kazi cha kuwajengea uwezo wasanii, Viongozi wa Vyama vya Mpira wa pete - Netboli Tanzania Bara na Zanzibar (CHANETA & CHANEZA) wakati wa kikao kilichofanyika leo Oktoba 01, 2026 katika Ofisi ndogo ya Makamu wa Rais, Luthuli Jijini Dar es Salaam.

Ofisi ya Makamu wa Rais imefanya kikao kazi cha kuwajengea uwezo wasanii, Viongozi wa Vyama vya Mpira wa pete - Netboli Tanzania Bara na Zanzibar (CHANETA & CHANEZA) wakati wa kikao kilichofanyika leo Oktoba 01, 2026 katika Ofisi ndogo ya Makamu wa Rais, Luthuli Jijini Dar es Salaam.

Katika Kikao kazi hicho Bi. Pili Rashid Mgunda, Mwakilishi wa Katibu Mkuu CHANETA na Bw. Fredrick Michael Apikwa Katibu CHANEZA, waliahidi kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Rais katika kutoa Elimu ya Muungano kabla, wakati na baada ya Michezo hiyo.”Michezo ni fursa ya pekee ambayo inawakutanisha watu wa rika mbalimbali hivyo tunaiomba Ofisi ya Makamu wa Rais iwe tayari kutuunga mkono wakati wa maandalizi na Wakati wa Michezo ya mpira wa Pete kwa kutupatia Vipeperushi, Mabango ya Matangazo na hata jezi ambazo zitakuwa na Jumbe za Muungano” amesema, Pili Mgunda kwa niaba ya Katibu wa CHANETA.

Akiunga Mkono hoja hiyo Mkurugenzi wa Muungano Dkt. Juma Salum alisema timu ya Mpira wa Pete ya Ofisi ya Makamu wa Rais itashiriki Mashindano yatakayofanyika hivi karibuni Mkoani Tanga na kuchukua ubingwa, aidha Ofisi ya Makamu wa Rais itatumia fursa hiyo adhimu kutoa Elimu ya Muungano.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi

slot gacor