
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira Mhe. Jackson Kiswaga akiongoza kikao wakati Ofisi ya Makamu wa Rais ikiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mpango na bajeti kwa mwaka wa fedha 2025/26 na makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2026/27 kwenye Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira, Machi 23, 2026.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Richard Muyungi akizungumza wakati wa uwasilishwaji wa taarifa ya utekelezaji wa mpango na bajeti kwa mwaka wa fedha 2025/26 na makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2026/27 kwenye Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira, Machi 23, 2026.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Festo Dugange akiwa katika kikao cha kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mpango na bajeti kwa mwaka wa fedha 2025/26 na makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2026/27 kwenye Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira, Machi 23, 2026.





===============================================================================================================
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira wakiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Jackson Kiswaga wameridhishwa na utekelezaji wa majukumu ya usimamizi wa mazingira katika Ofisi ya Makamu wa Rais ambao umechangia maendeleo endelevu.
Hayo yamejiri leo Machi 23, 2026 jijini Dodoma wakati wa kikao cha kupokea taarifa ya utekelezaji wa mpango na bajeti kwa mwaka 2025/26 na makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2026/27 kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira.
Akizungumza wakati wa kikao hicho, Mhe. Kiswaga alisema kuwa kamati hiyo inapongeza Ofisi hiyo kwa kuibadili jamii kuachana na vitendo vya uharibifu wa mazingira kupitia miradi mbalimbali inayotekelezwa katika baadhi ya maeneo nchini.
Alisema kuwa kuna mabadiliko makubwa katika maeneo mengi nchini hususan ambayo miradi ya mazingira inatekelezwa kwani inawawezesha wananchi kuacha kukata miti na kuhifadhi misitu na kufanya shughuli za kujipatia kipato bila kuathiri mazingira.
“Tunawapongeza Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kazi nzuri pamoja na kuwa hawana fedha nyingi wao wanafanya kazi ya uratibu wa shughuli zote za mazingira ikiwemo hii miradi tunayoitembelea,“ alisema.
Aidha, Mhe. Kiswaga ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kalenga alisisitiza kuwa Ofisi itanue wigo wa utoaji wa elimu kwa umma kuhusu kulinda na kuhifadhi mazingira ishuke ngazi ya chini hasa vijijini kwa wananchi kwakuwa uelewa wa wananchi bado mdogo.
Akitolea ufafanuzi wa hoja mbalimbali za wajumbe wa kamati, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni alisema katika kuhakikisha agenda ya hifadhi ya mazingira inaseonga mbele na kuwa endelevu, Ofisi hiyo imekuja na mtazamo wa kufanya mageuzi ya kimkakati, kisheria na kitaasisi.
Alifafanua kuwa mchakato wa kulipa hadhi Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kuwa Mamlaka kamili ili kuwa na meno (nguvu kubwa kisheria) ya kukabiliana na uharibifu wa mazingira uko katika hatua nzuri.
“Kisheria, tunaamini mabadiliko hayo ya kuifanya NEMC kuwa na mamlaka yataleta impact (ufanisi) hivyo tunaendelea na hatua mbalimbali za mchakato katika mabadiliko ya sheria ili lifike mapema zaidi bungeni, niwaombe waheshimiwa wajumbe tuendelee kuwa na subira kwani jambo hili linahusisha mamlaka mbalimbali za Serikali katika kufikia hatua ya mwisho kwani maamuzi yatakayofikiwa ni kwa ajili ya wananchi,“ alisisitiza Mhandisi Masauni.
Pamoja na hayo alisema kuwa tayari NEMC wameanza ujenzi wa Makao Makuu ya Kanda ya Ziwa/Magharibu yaliyopo mkoani Geita ambayo pia kinajengwa kituo cha umahiri.
Alisema eneo hilo litakuwa ni sehemu ya kutoa elimu ya hifadhi ya mazingira hususan kwa wachimbaji wadogo wa dhahabu kuhusu athari za matumizi ya zebaki katika uchenjuaji.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Richard Muyungi alisema ili kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wa fedha za miradi, Serikali imeingia mikataba ya kimataifa 12 ambayo Ofisi inasimamia ili kupata rasilimali hizo.
Aliongeza kuwa ipo Mifumo minne ambayo ni Mfuko wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi (AF) ambao kuanzia mwaka 2026 NEMC itaanza kupokea fedha kwa ajili mazingira, Mfuko wa Hasara na Uharibifu, Mfuko wa Mabadiliko ya Tabianchi ya Kijani (GCF) na Mfuko wa Mazingira wa Dunia (GEF) ambao umeleta fedha nyingi kwa kuda mrefu hasa miradi za miradi mbalimbali na
Hivyo, Dkt. Muyungi alisema pamoja na changamoyo kadhaa, Mifuko hiyo imekuwa ikileta mafanikio kwa kusaidia kutatua changamoto za mabadiliko ya tabianchi.