Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu Rasmi ya Ofisi ya Makamu wa Rais

Makamu wa Rais aishukuru IMF kwa kuiunga mkono Tanzania
Jan 28, 2025
Makamu wa Rais aishukuru IMF kwa kuiunga mkono Tanzania
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akifanya Mazungumzo na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Bw. Bo Li, mazungumzo yaliyofanyika kando ya Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Afrika unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam. Tarehe 28 Januari 2025.
Na Robert Hokororo

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Bw. Bo Li, mazungumzo yaliyofanyika kando ya Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Afrika unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam leo tarehe 28 Januari 2025.

Katika Mazungumzo hayo, Makamu wa Rais amelishukuru Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) kwa kuendelea kuiunga mkono Tanzania kupitia programu mbalimbali ikiwemo dirisha la mikopo nafuu ya nyongeza ya kuchochea kasi ya kuimarisha uchumi baada ya Janga la UVIKO-19 na misukosuko itokanayo na vita (Extended Credit Facility - ECF) pamoja  na programu ya kuimarisha uwezo wa nchi kukabiliana changamoto zitokanazo na athari za mabadiliko ya tabianchi (Resilience and Sustainability Facility-RSF). 

Amesema kupitia programu hizo, zimechangia ukuaji wa uchumi, kudhibiti mfumuko wa bei na ongezeko la mikopo kwa sekta binafsi. 

Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Bw. Bo Li ameipongeza Tanzania kwa kuimarisha uchumi na kufanikisha utekelezaji wa programu za ushirikiano ikiwamo programu kupitia ECF na RSF. Aidha ameipongeza Tanzania kwa kutekeleza vyema programu ya ECF na kupata alama za juu katika tathimini ya nne. 

Aidha, Bw. Li aameipongeza Tanzania kwa kuwa nchi ya mfano iliyochaguliwa pamoja na Madagascar kutekeleza mpango kabambe wa utafutaji wa fedha za mazingira kutoka kwa wadau mbalimbali ikiwamo sekta binafsi, washirika wa maendeleo na AZAKI. 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi