Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu Rasmi ya Ofisi ya Makamu wa Rais

Makamu wa Rais: Serikali inathamini mchango wa Taasisi za Dini
Aug 08, 2026
Makamu wa Rais: Serikali inathamini mchango wa Taasisi za Dini
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akishiriki Ibada ya Misa Takatifu Maalum ya Wanajumuiya wa Uru Seminari, iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Parokia ya Kristo Mchungaji Mwema – Tabata Kimanga Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 08 Agosti 2026.
Na Robert Hokororo

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akishiriki Ibada ya Misa Takatifu Maalum ya Wanajumuiya wa Uru Seminari, iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Parokia ya Kristo Mchungaji Mwema – Tabata Kimanga Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 08 Agosti 2026.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akizungumza na Wanajumuiya wa Uru Seminari, mara baada ya kushiriki Ibada ya Misa Takatifu Maalum ya Wanajumuiya hao iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Parokia ya Kristo Mchungaji Mwema – Tabata Kimanga Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 08 Agosti 2026.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akiwa na Askofu wa Jimbo Katoliki Kigoma, Mhashamu Joseph Mlola, Mapadre katika picha ya pamoja na Wanajumuiya wa Uru Seminari, mara baada ya kushiriki Ibada ya Misa Takatifu Maalum ya Wanajumuiya hao iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Parokia ya Kristo Mchungaji Mwema – Tabata Kimanga Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 08 Agosti 2026.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akiwa na Askofu wa Jimbo Katoliki Kigoma, Mhashamu Joseph Mlola, Mapadre katika picha ya pamoja na Wanajumuiya wa Uru Seminari, mara baada ya kushiriki Ibada ya Misa Takatifu Maalum ya Wanajumuiya hao iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Parokia ya Kristo Mchungaji Mwema – Tabata Kimanga Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 08 Agosti 2026.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akiwa na Askofu wa Jimbo Katoliki Kigoma, Mhashamu Joseph Mlola, katika picha ya pamoja na Walimu wa Uru Seminari, mara baada ya kushiriki Ibada ya Misa Takatifu Maalum ya Wanajumuiya wa Shule ya Uru Seminari iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Parokia ya Kristo Mchungaji Mwema – Tabata Kimanga Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 08 Agosti 2026.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akiwa na Askofu wa Jimbo Katoliki Kigoma, Mhashamu Joseph Mlola mara baada ya kushiriki Ibada ya Misa Takatifu Maalum ya Wanajumuiya wa Uru Seminari, iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Parokia ya Kristo Mchungaji Mwema – Tabata Kimanga Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 08 Agosti 2026.

=================================================================================

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amesema Serikali itaendelea kuthamini mchango wa Taasisi za Dini ambazo kwa namna ya pekee zimekuwa zikishiriki katika kutoa mchango kwenye sekta za Afya na Elimu hapa nchini.

 

Makamu wa Rais amesema hayo mara baada ya kushiriki Ibada ya Misa Takatifu Maalum ya Wanajumuiya wa Uru Seminari, iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Parokia ya Kristo Mchungaji Mwema – Tabata Kimanga Jijini Dar es Salaam. Amesema kwa miaka mingi na kwa asilimia kubwa Taasisi za dini zimechangia katika utoaji wa huduma za elimu na afya, hivyo Serikali itaendelea kushirikiana na Taasisi hizo ili kufanikiwa zaidi katika kulijenga Taifa.

 

Makamu wa Rais amesema Malezi yanayotolewa katika Taasisi za elimu za dini ikiwemo Shule ya Uru Seminari ambayo husisitiza Sala, Kazi na Masomo yanapaswa kutiliwa mkazo katika malezi ya vijana wa sasa. Amesema vijana watakavyoweza kumjua Mungu, kufanya kazi kwa bidii pamoja na kupata elimu wataweza kulijenga vema Taifa kupitia ujuzi na hivyo kuepusha tabia za kupata kipato kupitia njia zisizo sahihi.

 

Makamu wa Rais amewashukuru, walimu, walezi na wanafunzi waliopata elimu Uru Seminari kwa ushirikiano na malezi mazuri ambayo yalifundisha kumtumikia Mungu pamoja na Wanadamu.

 

Amewasihi Wanajumuiya ya Uru Seminari kuendeleza umoja na kuhakikisha unakuwa wenye tija kwa Taifa, pamoja na kuendelea kuiombea nchi na Viongozi wake.

 

Ibada ya Misa Takatifu ya Wanajumuiya wa Uru Seminari, imeongozwa na Askofu wa Jimbo Katoliki Kigoma, Mhashamu Joseph Mlola. 

 

Akitoa mahubiri kwa Wanajumuiya WA Uru Seminari , Askofu Mlola amewasihi kukumbuka wito muhimu walionao wa kupeleka tunu njema ya Maisha ya kiimani kuishi kwa kumpendeza Mungu pamoja na wanadamu. Amesema ni muhimu kuwa mstari wa mbele kupeleka matumaini, ukweli, amani na haki. 

 

Pia, Askofu Mlola amewasihi kuhakikisha uwepo wa kila mwanajumuiya wa Uru Seminari analeta upendo na matumaini, kwa kutambua huo ni wito kwao waliolelewa na kufundishwa katika malezi na maadili mema.

 

Uru Seminari ni Shule inayomilikiwa na Kanisa Katoliki Jimbo Katoliki la Moshi, chini ya Shirika la Mitume wa Yesu inayopatikana Wilaya ya Moshi Mkoani Kilimanjaro.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi

slot gacor