Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu Rasmi ya Ofisi ya Makamu wa Rais

Menejimenti ya Ofisi ya Makamu wa Rais yakutana kujadili muelekeo 2026/27
Aug 05, 2026
Menejimenti ya Ofisi ya Makamu wa Rais yakutana kujadili muelekeo 2026/27
Naibu Katibu Mkuu (Mazingira), Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Maduhu Isaac Kazi, akitoa hotuba ya ufunguzi wakati wa kikao kazi cha tathmini ya utekelezaji wa shughuli za Ofisi ya Makamu wa Rais kwa mwaka wa fedha 2025/26 na kujadili mwelekeo wa utekelezaji wa majukumu kwa mwaka wa fedha 2026/27, kilichofanyika leo, Agosti 4, 2026, katika Hoteli ya Pan African Postal Union (PAPU), jijini Arusha.
Na Robert Hokororo

Naibu Katibu Mkuu (Mazingira), Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Maduhu Kazi, akiongoza kikao kazi cha tathmini ya utekelezaji wa shughuli za Ofisi ya Makamu wa Rais kwa mwaka wa fedha 2025/26 na kujadili mwelekeo wa utekelezaji wa majukumu kwa mwaka wa fedha 2026/27, kilichofanyika leo, Agosti 4, 2026, katika Hoteli ya Pan African Postal Union (PAPU), jijini Arusha.

Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango, Bw. Said Mabie, akiwasilisha taarifa ya mwelekeo wa bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Rais kwa mwaka wa fedha 2026/27 wakati wa kikao kazi kilichoongozwa na Naibu Katibu Mkuu (Mazingira), Dkt. Maduhu Isaac Kazi, kilichofanyika leo, Agosti 4, 2026, katika Hoteli ya Pan African Postal Union (PAPU), jijini Arusha. 

Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira, Bi. Kemilembe Mutasa, akiwasilisha taarifa kuhusu utekelezaji wa shughuli za mazingira wakati wa kikao kazi kilichoongozwa na Naibu Katibu Mkuu (Mazingira), Dkt. Maduhu Isaac Kazi, kilichofanyika leo, Agosti 4, 2026, katika Hoteli ya Pan African Postal Union (PAPU), jijini Arusha. 

Mkurugenzi wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini, Bw. Obadiah Nyagiro, akiwasilisha taarifa ya ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa shughuli za Ofisi ya Makamu wa Rais kwa mwaka wa fedha 2025/26 wakati wa kikao kazi kilichoongozwa na Naibu Katibu Mkuu (Mazingira), Dkt. Maduhu Isaac Kazi, kilichofanyika leo, Agosti 4, 2026, katika Hoteli ya Pan African Postal Union (PAPU), jijini Arusha. 

Naibu Katibu Mkuu (Mazingira), Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Maduhu Isaac Kazi (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Menejimenti ya Ofisi ya Makamu wa Rais mara baada ya kuongoza kikao kazi cha tathmini ya utekelezaji wa shughuli za Ofisi kwa mwaka wa fedha 2025/26 na kujadili mwelekeo wa utekelezaji wa majukumu kwa mwaka wa fedha 2026/27, kilichofanyika leo, Agosti 4, 2026, katika Hoteli ya Pan African Postal Union (PAPU), jijini Arusha. Waliokaa kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Adela Mkude, na kulia ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini, Bw. Obadiah Nyagiro

=========================================================================================================

Naibu Katibu Mkuu (Mazingira), Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Maduhu Kazi, Agosti 4, 2026 ameongoza kikao kazi kilichofanyika katika Hoteli ya Pan African Postal Union (PAPU), jijini Arusha, kilicholenga kufanya tathmini ya utekelezaji wa shughuli za Ofisi ya Makamu wa Rais kwa mwaka wa fedha 2025/26 na kujadili mwelekeo wa utekelezaji wa majukumu kwa mwaka wa fedha 2026/27 katika kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Kikao hicho kimewakutanisha viongozi na watendaji wa Ofisi ya Makamu wa Rais kwa lengo la kutathmini utekelezaji wa mipango na bajeti, kubaini mafanikio yaliyopatikana, changamoto zilizojitokeza pamoja na kuweka mikakati ya kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya Ofisi kwa kipindi kijacho.

Katika kikao hicho, washiriki walijadili taarifa ya ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Ofisi ya Makamu wa Rais kwa mwaka wa fedha 2025/26, iliyowasilishwa na Mkurugenzi wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini, Bw. Obadiah Nyagiro. Taarifa hiyo ilieleza hali ya utekelezaji wa mipango na shughuli mbalimbali za Ofisi, mafanikio yaliyofikiwa, changamoto zilizobainika pamoja na maeneo yanayohitaji kuimarishwa ili kuongeza ufanisi na tija katika utekelezaji wa majukumu.

Aidha, kikao kilipokea na kujadili taarifa ya mwelekeo wa bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Rais kwa mwaka wa fedha 2026/27, iliyowasilishwa na Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango, Bw. Said Mabie. Wasilisho hilo lilijikita katika vipaumbele vya upangaji wa bajeti, matumizi bora ya rasilimali za Serikali na uelekezaji wa fedha katika maeneo ya kimkakati yatakayochangia utekelezaji wa majukumu ya Ofisi sambamba na kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Washiriki pia walipokea taarifa kuhusu utekelezaji wa kazi mbalimbali za mazingira iliyowasilishwa na Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira, Bi. Kemilembe Mutasa. Taarifa hiyo ilieleza maendeleo ya utekelezaji wa majukumu ya Idara ya Mazingira, ikiwemo uratibu wa usimamizi wa mazingira, utekelezaji wa sera na sheria za mazingira, uratibu wa masuala ya mabadiliko ya tabianchi, usimamizi wa tathmini za athari kwa mazingira pamoja na kuimarisha ushirikiano na wadau mbalimbali katika kuhifadhi mazingira na kuhakikisha matumizi endelevu ya rasilimali za asili.

Kikao hicho ni sehemu ya utaratibu wa Ofisi ya Makamu wa Rais wa kufanya tathmini ya utendaji wa kazi, kuimarisha mifumo ya ufuatiliaji na tathmini, kuongeza uwajibikaji katika utekelezaji wa mipango na kuhakikisha maandalizi ya mwaka wa fedha 2026/27 yanazingatia vipaumbele vya Taifa na malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi

slot gacor