Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu Rasmi ya Ofisi ya Makamu wa Rais

Tanzania, GEF kuimarisha ushirikiano katika uhifadhi wa bioanuwai
Oct 28, 2026
Tanzania, GEF kuimarisha ushirikiano katika uhifadhi wa bioanuwai
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (wa pili kulia) akimsikiliza Kiongozi wa Kimataifa wa Mfumo wa Chakula na Matumizi ya Ardhi kutoka GEF, Dkt. Peter Umunay walipokutana kwa ajili ya mazungumzo pembezoni mwa Mkutano wa 17 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Kimataifa wa Hifadhi ya Bioanuai unaofanyika jijini Yerevan, Armenia, Oktoba 28, 2026. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu (Mazingira), Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Maduhu Kazi pamoja na Mkurugenzi Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Bi. Farhat Mbarouk
Na Robert Hokororo

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (kushoto) akisalimiana na Afisa Mtendaji Mkuu na Mwenyekiti wa Mfuko wa Mazingira Duniani (GEF), Diego Mesa Puyo, walipokutana kwa ajili ya mazungumzo pembezoni mwa Mkutano wa 17 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Kimataifa wa Hifadhi ya Bioanuai unaofanyika jijini Yerevan, Armenia, Oktoba 28, 2026.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (katikati) akimsikiliza Kiongozi wa Kimataifa wa Mfumo wa Chakula na Matumizi ya Ardhi kutoka GEF, Dkt. Peter Umunay walipokutana kwa ajili ya mazungumzo pembezoni mwa Mkutano wa 17 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Kimataifa wa Hifadhi ya Bioanuai unaofanyika jijini Yerevan, Armenia, Oktoba 28, 2026. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu (Mazingira), Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Maduhu Kazi.

===============================================================================================================

Tanzania imezidi kuimarisha ushirikiano wake na Mfuko wa Mazingira Duniani (GEF) ili kuendeleza miradi inayotekelezeka na kuimarisha juhudi za uhifadhi wa bioanuwai nchini.

 

Katika mapendekezo yake, Tanzania imeeleza umuhimu wa kuanzisha mazungumzo ya kitaalamu kati ya GEF, Ofisi ya Makamu wa Rais na taasisi husika za kisekta, ikiwemo taasisi zinazotekeleza miradi, ili kubaini maeneo yenye uhitaji wa fedha na kuweka vipaumbele vya uwekezaji katika uhifadhi wa mazingira.

 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni ameyasema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Afisa Mtendaji Mkuu na Mwenyekiti wa GEF, Diego Mesa Puyo, pembezoni mwa Mkutano wa 17 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Kimataifa wa Hifadhi ya Bioanuai uliofanyika jijini Yerevan, Armenia, Oktoba 28, 2026.

 

Mhe. Masauni amesema Tanzania imeomba GEF kutoa mwongozo kuhusu namna ya kuoanisha miradi inayopendekezwa na mwelekeo wa programu za GEF, vigezo vya kustahili kupata ufadhili katika maeneo husika, pamoja na taratibu zinazopaswa kufuatwa katika mzunguko wa maandalizi na utekelezaji wa miradi.

 

Katika hatua nyingine, Tanzania imependekeza kuwepo kwa mikakati ya pamoja ya kuhamasisha rasilimali fedha kutoka Serikalini, kwa washirika wa maendeleo, mashirika ya uhifadhi na sekta binafsi inayowajibika. 

 

Amesema hatua hiyo inalenga kupanua wigo wa vyanzo vya fedha na kuongeza uwezo wa kugharamia miradi ya uhifadhi wa bioanuwai na mazingira kwa muda mrefu.

 

Tanzania pia imehimiza majadiliano kuhusu mifumo endelevu ya ufadhili wa uhifadhi, ikiwemo mifuko ya dhamana ya uhifadhi, malipo kwa huduma za mifumo ikolojia na uwekezaji unaochangia uhifadhi wa mazingira, huku ukizingatia hatua stahiki za kulinda mazingira na maslahi ya jamii.

 

Sambamba na hayo, imeiomba GEF kuongeza msaada wa kitaalamu na kitaasisi kwa Ofisi ya Uratibu ya Kituo cha Kitaifa cha Uendeshaji wa GEF nchini Tanzania ili kuimarisha uwezo wake wa kuandaa miradi yenye uwezekano wa kupata ufadhili na kutekelezeka kwa ufanisi.

 

Msaada huo unatarajiwa kujumuisha maandalizi ya miradi, ukusanyaji wa takwimu za msingi, tafiti za upembuzi yakinifu na uandaaji wa maandiko ya awali ya miradi yaliyo tayari kwa uwekezaji.

 

Kwa ujumla, mapendekezo hayo yanalenga kuimarisha uratibu kati ya taasisi za Serikali na wadau wa maendeleo, kuongeza upatikanaji wa rasilimali fedha na kujenga uwezo wa kitaasisi ili kuhakikisha miradi ya uhifadhi wa bioanuwai inapata maandalizi yanayostahili na fursa pana zaidi za ufadhili.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi

slot gacor