Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu Rasmi ya Ofisi ya Makamu wa Rais

Tanzania kuvuna bilioni 108/- za uhifadhi wa mazingira
Oct 12, 2026
Tanzania kuvuna bilioni 108/- za uhifadhi wa mazingira
Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Maduhu Kazi akifungua Mkutano wa kitaifa wa Uzinduzi Mzunguko wa Tisa wa utoaji wa fedha za mazingira kutoka Mfuko wa Mazingira wa Dunia ‘Global Environment Facility’ (GEF) unaofanyika jijini Dar es Salaam leo Oktoba 12, 2026.
Na Robert Hokororo

Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Maduhu Kazi akifungua Mkutano wa kitaifa wa Uzinduzi Mzunguko wa Tisa wa utoaji wa fedha za mazingira kutoka Mfuko wa Mazingira wa Dunia ‘Global Environment Facility’ (GEF) unaofanyika jijini Dar es Salaam leo Oktoba 12, 2026.

Washiriki mbalimbali wakiwa katika Mkutano wa kitaifa wa Uzinduzi Mzunguko wa Tisa wa utoaji wa fedha za mazingira kutoka Mfuko wa Mazingira wa Dunia ‘Global Environment Facility’ (GEF) unaofanyika jijini Dar es Salaam leo Oktoba 12, 2026.

===============================================================================

Tanzania inatarajia kupokea Dola za Kimarekani milioni 41.06 (shilingi bilioni 108.5) kutoka Mfuko wa mazingira Duniani (GEF) zitakazosaidia katika kufanikisha shughuli za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kusukuma mbele agenda ya utunzaji wa mazingira kwa ujumla.

 

Hayo yamebainishwa na Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Maduhu Kazi wakati akifungua Mkutano wa kitaifa wa Uzinduzi Mzunguko wa Tisa wa utoaji wa fedha za mazingira kutoka Mfuko wa Mazingira wa Dunia ‘Global Environment Facility-9’ (GEF)-9.

 

Akifungua mkutano huo kwa niaba ya Katibu Mkuu Dkt. Richard Muyungi, Dkt. Kazi alisema uhusiano mzuri unaojengwa na Tanzania na wadau umechangia nchi kuendelea kupata fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya kuhifadhi mazingira.

 

Itakumbukwa katika awamu ya nane ya mzunguko wa utoaji wa fedha za hifadhi ya mazingira, Tanzania ilipokea jumla ya dola milioni 53.5 (shilingi bilioni 141.3), uwekezaji ambao umechangia kuimarisha uwezo wa kitaasisi, kusaidia maisha ya jamii, kuboresha ustahimilivu wa mfumo ikolojia na kuendeleza utekelezaji wa vipaumbele vya kitaifa vya mazingira.

 

Dkt. Kazi alieleza kuwa fedha hizo zitasaidia kusogeza mbele agenda ya mazingira hususan katika utekelezaji wa miradi ya usimamizi wa mazingira uhifadhi wa bayoanuwai, kupunguza na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, uharibifu wa ardhi, usimamizi endelevu wa misitu, kemikali na usimamizi wa taka, na ulinzi wa maji ya kimataifa.

 

“Kiujumla masuala ya mazingira yapo sehemu kubwa ya utekelezaji wa Dira 2050 na ni nguzo ya tatu hii ni kwasababu katika masuala ya mazingira tunatakiwa kujenga uchumi na huwezi kuendelea wakati mazingira yanaharibika, hivyo fedha hizi zitakuwa msaada mkubwa,” alisema.

 

Chini ya mzunguko uliopita wa uongezaji wa rasilimali wa GEF-8 (2022–2026), Tanzania ilipokea jumla ya Dola za Marekani milioni 33.5 kupitia mgao wa GEF STAR, ambao ulielekezwa katika maeneo makuu matatu.

 

Maeneo hayo ni Bioanuwai lilipata sehemu kubwa zaidi ya Dola milioni 23.9, likifuatiwa na eneo la Uharibifu wa Ardhi (Dola milioni 4.8) na eneo la Mabadiliko ya Tabianchi (Dola milioni 4.8). 

 

Mbali na mgao wa STAR, Tanzania ilitengewa Dola milioni 20 kupitia Mfuko wa Nchi Zilizo Nyuma Kimaendeleo (LDCF) kwa ajili ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi, jambo lililofanya jumla ya manufaa kutoka GEF-8 kufikia takriban Dola milioni 53.5. 

Dkt. Kazi alisema kuwa rasilimali zote zilizotengwa tayari zimepangwa kikamilifu na kuidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kiasi hicho chote kilichotengwa.

Hivyo, aliishukuru Sekretarieti ya GEF, washirika wa maendeleo, taasisi za Serikali na wadau wote kwa msaada wao unaoendelea na ushirikiano katika kuendeleza ajenda ya mazingira ya Tanzania.

Kwa upande wake Bw. Yusuph Tango ambaye ni mratibu wa miradi kutoka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) alisema wakala huo umenufaika na miradi zaidi ya 20 kupitia mpango huo.Alisema TFS ambayo ina dhamana ya kusimamia rasiliamali za misitu na nyuki katika mkutano huo inaonesha namna inavyonufaika na fedha za GEF ambazo zinasaidia kutekeleza miradi hiyo.

Bw. Tango alisema TFS inalenga kubainisha fursa za ufadhili wa misitu na nyuki ambazo zitakuwa chachu ya kuboresha na kukuza sekta ya utalii ambayo inaingizia kipato nchi.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi

slot gacor