Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu Rasmi ya Ofisi ya Makamu wa Rais

Tanzania yasisitiza umuhimu wa usimamizi wa mazingira ya bahari
Oct 09, 2026
Tanzania yasisitiza umuhimu wa usimamizi wa mazingira ya bahari
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Misitu, Uvuvi na Mazingira wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mhe. Narend Singh wakati wa Mkutano wa Uwili pembezoni mwa kuhusu Mkutano wa 12 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Nairobi (COP12) unaoendelea Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.
Na Robert Hokororo

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Misitu, Uvuvi na Mazingira wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mhe. Narend Singh wakati wa Mkutano wa Uwili pembezoni mwa kuhusu Mkutano wa 12 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Nairobi (COP12) unaoendelea Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.

=======================================================================================================================

Tanzania imesisitiza umuhimu wa usimamizi jumuishi wa mazingira ya pwani na bahari, ikieleza kuwa afya ya mifumo ya ikolojia ya baharini ni msingi wa uvuvi, utalii, ustahimilivu dhidi ya mabadiliko ya tabianchi na maendeleo ya uchumi wa buluu kwa muda mrefu.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni ameyasema hayo leo Oktoba 9, 2026 dhidi ya Naibu Waziri wa Misitu, Uvuvi na Mazingira wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mhe. Narend Singh wakati wa Mkutano wa Uwili pembezoni mwa kuhusu Mkutano wa 12 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Nairobi (COP12) unaoendelea Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.

Amesema changamoto zinazohitaji kushughulikiwa ni pamoja na uchafuzi wa mazingira ya bahari, taka za plastiki, uharibifu wa makazi ya viumbe vya baharini, athari za mabadiliko ya tabianchi na ushindani unaoongezeka katika matumizi ya maeneo ya pwani.

“Katika eneo hili, uzoefu wa Afrika Kusini katika usimamizi jumuishi wa pwani, uanzishaji na usimamizi wa maeneo tengefu ya baharini, ufuatiliaji wa mazingira na uhifadhi wa rasilimali za bahari unaweza kuwa na manufaa kwa Tanzania.”

Ushirikiano huo unaweza kusaidia kuimarisha usimamizi wa shughuli za maendeleo huku ukihakikisha kuwa uhifadhi wa mazingira unaenda sambamba na mahitaji ya kiuchumi na kijamii ya wananchi.

Mbali na uwekezaji na uhifadhi, Tanzania inataka kuimarisha ushirikiano na Afrika Kusini katika sayansi ya bahari, teknolojia na ubunifu ili kuongeza matumizi ya ushahidi wa kisayansi katika upangaji, usimamizi wa mazingira na maendeleo ya viwanda vinavyotegemea rasilimali za bahari.

Maeneo yanayoweza kunufaika na ushirikiano huo ni pamoja na mifumo ya ufuatiliaji wa bahari, utafiti wa viumbe na mifumo ya ikolojia ya baharini, teknolojia za ufugaji wa viumbe vya majini na teknolojia ya kibayolojia inayotokana na rasilimali za bahari.

Ushirikiano kati ya Tanzania na Afrika Kusini katika uchumi wa bahari una nafasi ya kuwa kichocheo muhimu cha uwekezaji, ajira, ubunifu na maendeleo endelevu ya jamii za pwani.

Kupitia ubadilishanaji wa uzoefu, teknolojia na utaalamu, nchi hizo zinaweza kuimarisha matumizi endelevu ya rasilimali za bahari, kuongeza thamani ya mazao ya uvuvi, kukuza utalii wa baharini na kuboresha huduma zinazohusiana na bandari na usafiri wa majini.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi

slot gacor