Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu Rasmi ya Ofisi ya Makamu wa Rais

Waziri Masauni ahimiza umuhimu wa kupanda miti
May 15, 2026
Waziri Masauni ahimiza umuhimu wa kupanda miti
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni akipanda mti pembezoni mwa Mto Mkondoa uliopo Kata ya Kasiki Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro, Mei 15, 2026.
Na Robert Hokororo

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni akiwasili stesheni ya Reli ya Kisasa Wilaya ya Kilosa kwa ajili ya kuongoza zoezi la upandaji miti wilayani humo mkoani Morogoro, zoezi lililofanyika Mei 15, 2026. Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Mhe. Shaka Hamdu Shaka.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (katikati) akiongozana na Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Mhe. Shaka Hamdu Shaka alipokuwa kwenye ziara ya kikazi wilayanii humo, Mei 15, 2026.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (katikati) akimsikiliza Msimamizi wa Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu Kilosa Bw.Christian Kipondya wakati wa ziara yake ya kikazi Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro, Mei 15,2026. Kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Mhe. Shaka Hamdu Shaka.

Naibu Katibu Mkuu (Mazingira), Ofisi ya Makamu wa Rais, Balozi Baraka Luvanda akipanda mti pembezoni mwa Mto Mkondoa uliopo Kata ya Kasiki Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro, ikiwa moja ya shughuli zilizopangwa na Ofisi ya Makamu wa Rais kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani.

================================================================================================================

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe. Mhandisi Hamad Masauni amesema Usimamizi na uhifadhi wa mazingira hauwezi kufanikiwa kwa kauli au sera peke yake, bali kwa vitendo vinavyoonekana katika ngazi zote ikiwemo shughuli za kupanda miti na kuitunza.

Amesema maono na Matarajio ya Dira 2050 ni makubwa na yanahitaji ubunifu mkubwa katika kufanya kazi ili kufikia matarajio hasa katika mikakati mahsusi ya hifadhi na ustahimilivu wa mabadiliko ya tabianchi.

Waziri Masauni ameyasema hayo Mei 15, 2026 wilayani Kilosa mkoani Morogoro kwenye zoezi la upandaji miti ili kuhakikisha mazingira yanabaki kuwa salama kutokana na uoto wa asili ikiwa moja shughuli zilizopangwa na Ofisi ya Makamu wa Rais kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani itakayofanyika Juni 5 mwaka huu ambapo kitaifa itafanyika mkoani Dodoma.

Amesema Dira ya Taifa ya mwaka 2050 ina nguzo kuu tatu na miongoni mwa nguzo hizo ni suala zima la uhifadhi wa mazingira na ustahimilivu wa mabadiliko ya tabianchi jambo ambalo kila mmoja anapaswa kulitazama kwa upana wake.

"Haya tunayoyaona hapa kama vile athari za mafuriko, hali ya hewa isiyotabilika inayosababisha ukame na madhara mengine mengi miongoni mwa sababu zake ni mabadiliko ya tabianchi, hivyo kama taifa ni lazima tutoe kipaumbele katika kuhakikisha athari za mabadiliko ya tabianchi tunazihimili," amesema Masuni.

Ameongeza kuwa mtu anaweza asione faida ya upandaji miti lakini ukweli ni kuwa miti hiyo inafaida kuwa katika suala zima la upandaji miti hasa kwa kizazi kijacho cha miaka 50 ijayo kwani ndiyo wenye Tanzania ya baadaye.

Aidha Waziri Masauni aliipongeza Wilaya ya Kilosa na mkoa mzima wa Morogoro kwa kuwahusisha wananafuzi wa shule za msingi na sekondari katika suala zima la upandaji miti na utunzaji mazingira.

Mhe. Masauni aliambatana na viongozi mbalimbali kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais akiwemo, Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Balozi Baraka Luvanda ambaye alieleza kuwa zoezi hilo lilianza tangu jana mkoani humo huku zaidi ya miti elfu arobaini ikipandwa.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Mhe. Shaka Hamdu Shaka kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Morogoro alisema kuwa wilaya hiyo imejiwekea malengo ya kupanda miti milioni 1.5 na kwamba zoezi hilo limekuwa likifanyika kila mwaka kwa mfululizo wa miaka mitano.

Mhe. Shaka amesema kuwa wilaya yake mara kwa mara imekuwa ikikumbwa na mafuriko na kwamba katika kukabiliana na hali hiyo, serikali imedhamilia kujenga mabwawa ya maji katika maeneo ya mto Mkondoa ili kuweza kudhibiti mafuriko, hivyo zoezi la upandi miti hiyo kutasaidia kulinda na kuhifidhi bwawa hilo na hivyo kuchochea maendeleo mbalimbali ya kiuchumi.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi

slot gacor