Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius John Ndejembi akishuhudia utiaji Saini leseni za utafutaji wa mafuta na gesi katika vitalu vya Mnazi bay north, West Songo songo, Eyasi wembere na Lindi – Mtwara, katika hafla iliyofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam, leo Tarehe 28 Oktoba 2026. Anayesaini ni Waziri wa Nishati Dkt. Juma Homera. Read More
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Reuben Kwagilwa (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki) Bw. Charles Kadonya (kulia) na Balozi wa Tanzania nchini Kenya Mhe. Dkt. Bernard Kibesse mara baada ya kuwasili jijini Kisumu, Kenya leo Oktoba 23, 2026 kushiriki Mkutano wa 24 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Kamisheni ya Bonde la Ziwa Victoria (LVBC) ulioanza Oktoba 19, 2026. Mhe. Kwagilwa anamwakilisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni. Read More
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni, akizungumza wakati akifungua Jukwaa la Soko la Kaboni na Uwekezaji Tanzania 2026, lililofanyika Jijini Dar es Salaam, Oktoba 22, 2026. Read More
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Richard Muyungi akifungua mafunzo ya Vijana wa Afrika kuhusu Majadiliano ya Mabadiliko ya Tabianchi yanayofanyika jijini Dar es Salaam yanayoshirikisha vijana kutoka takriban nchi 20. Read More
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Richard Muyungi akifungua kikao kati ya Ofisi hiyo na wasanii, waigizaji na watu wenye ushawishi cha kujadili mpango wa elimu kwa umma kuhusu Muungano kilichofanyika Oktoba 19, 2026 jijini Dar es Salaam. Read More
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi akishiriki Ibada ya Misa Takatifu ya Kumbukizi ya Miaka 27 ya kifo cha Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Parokia ya Epifania Jimbo Katoliki Sumbawanga, leo tarehe 14 Oktoba 2026. Read More
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza na waombolezaji mbalimbali, wakati akiwasilisha salamu za pole za Serikali katika msiba wa Bi. Kudra Salim Maghembe ambaye ni mama mzazi wa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Ngwaru Maghembe, wakati wa dua iliyofanyika katika makazi ya familia hiyo Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro, leo tarehe 12 Oktoba 2026. Read More
Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Maduhu Kazi akifungua Mkutano wa kitaifa wa Uzinduzi Mzunguko wa Tisa wa utoaji wa fedha za mazingira kutoka Mfuko wa Mazingira wa Dunia ‘Global Environment Facility’ (GEF) unaofanyika jijini Dar es Salaam leo Oktoba 12, 2026. Read More
Giza
Mwanga
Chaguo Msingi
Ndogo
Kawaida
Kubwa
slot gacor