
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Richard Muyungi akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais (hawapo pichani) waliopo Ofisi ndogo ya Zanzibar, Aprili 24, 2026.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Richard Muyungi akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais waliopo Ofisi ndogo ya Zanzibar, Aprili 24, 2026.
==========================================================================================
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Richard Muyungi amewatembelea na kuzungumza na watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais waliopo Ofisi ndogo ya Zanzibar, leo Aprili 24, 2026.
Katika ziara hiyo, Dkt. Muyungi amepokelewa na Mkurugenzi Msaidizi (Muungano) Ofisi ya Makamu wa Rais, Zanzibar Bi. Shumbana Taufiq.
Akizungumza na watumishi hao amewapongeza kwa utekelezaji wa majukumu yao hususan katika kuudumisha na kuuenzi Muungano.
Pia, Dkt. Muyungi amewahimiza kushiriki katika mazoezi na michezo kwa ujumla ili kujenga afya ya mwili.