Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu Rasmi ya Ofisi ya Makamu wa Rais

Masauni: Serikali yaendelea kuboresha mazingira Muungano ulete fursa
Aug 17, 2026
Masauni: Serikali yaendelea kuboresha mazingira Muungano ulete fursa
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni akiwasili viwanja vya Chuo cha Kiislamu Pemba kwa ajili ya Mahafali ya chuo hicho yaliyofanyika Agosti 16, 2026.
Na Robert Hokororo

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (kulia) akimkabidhi cheti mmoja wa wahitimu wa Chuo cha Kiislamu Pemba wakati wa Mahafali ya chuo hicho yaliyofanyika Agosti 16, 2026.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (kulia) akiteta jambo na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Hamad Chande wakati wa Mahafali ya Chuo cha Kiislamu Pemba yaliyofanyika Agosti 16, 2026.

===================================================================================

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni amesema Serikali imeendelea kuweka mazingira mazuri kwa vijana ili kunufaika katika fursa zinazopatikana kutokana na Muungano wa Tanzania.

 

Mhe. Masauni amesema moja ya eneo ambalo vijana wananufaika nalo ni kupitia sekta ya elimu ambapo wengi wanasoma kwa mkopo unaotokana na uwepo wa Muungano wa Tanzania.

 

Ameyasema hayo wakati wa Mahafali ya Chuo cha Kiislamu Pemba yaliyofanyika Agosti 16, 2026, akieleza kuwa vijana wanapaswa kuchangamkia fursa zilizopo ambazo ni nyingi kama vile ajira, elimu na biashara.

 

“Leo ni siku ya furaha, siku ya fahari, lakini pia ni siku ya kutafakari safari ndefu iliyowafikisha wahitimu wetu katika hatua hii muhimu ya maisha yao. Ni siku ambayo wazazi na walezi wanaona matunda ya juhudi, uvumilivu na kujitolea kwao.

 

Tunaipongeza Serikali ya Awamu ya Nane kwa kuendelea kutoa kipaumbele katika kuimarisha sekta ya elimu, kuboresha miundombinu ya elimu na, hususan, kuimarisha vyuo vya ualimu hapa Zanzibar. Juhudi hizi ni ushahidi wa dhamira ya Serikali ya kuwajengea uwezo vijana wetu ili na wao waende kufundisha wanafunzi wetu huko shuleni.

 

Amesema hakuna Taifa linaloweza kufikia maendeleo endelevu bila kuwa na watu wenye elimu, maarifa, ujuzi, ubunifu, maadili na uwezo wa kutatua changamoto zinazolikabili Taifa.

 

”Tunafahamu pia kwamba jukumu la kuendeleza elimu haliwezi kubebwa na Serikali pekee. Linahitaji ushirikiano wa Serikali zote mbili, taasisi za elimu, walimu, wazazi, viongozi, jamii na wadau mbalimbali.”

 

Ameongeza kuwa dunia tunayoiishi leo inabadilika kwa kasi kubwa kutokana na maendeleo ya sayansi, teknolojia na TEHAMA. Mabadiliko haya yanahitaji mwalimu anayejifunza na kujiboresha kila siku.

 

“Msiache kujifunza. Jifunzeni teknolojia mpya. Jifunzeni mbinu mpya za ufundishaji. Endeleeni kusoma. Endeleeni kujiongezea taaluma. Endeleeni kujenga uwezo wenu. Ninyi ndiyo mnaotarajiwa kuwa walimu wa kizazi cha kidijitali.”

 

Naye, Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Mhe. Mgeni Khatibu Yahya amesema wananchi wa Pemba wamekuwa shuhuda ya watu wanaonufaika na Muungano wa Tanzania kupitia miradi mbalimbali ikiwemo elimu.

 

Amesema moja ya manufaa ni pamoja na ujenzi wa majengo ya chou hicho ambapo fedha zake ni matunda ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi

slot gacor