Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu Rasmi ya Ofisi ya Makamu wa Rais

Dkt Muyungi awatia moyo wachezaji wa Netiboli Ofisi ya Makamu wa Rais
Apr 09, 2026
Dkt Muyungi awatia moyo wachezaji wa Netiboli Ofisi ya Makamu wa Rais
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais akizungumza na Kikosi cha Timu ya Mpira wa Pete ya Ofisi ya Makamu wa Rais kinachotarajia kushiriki Michuano ya Kombe la Mei Mosi 2026 mkoani Njombe.
Na Robert Hokororo

Kikosi cha Timu ya Mpira wa Pete ya Ofisi ya Makamu wa Rais kinatarajia kuondoka Dodoma kesho Aprili 10, 2026 kuelekea mkoani Njombe kwa ajili ya kushiriki Michuano ya Kombe la Mei Mosi inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi wiki ijayo.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Richard Muyungi amesema nidhamu na kujituma ndio silaha ya mafanikio ya ushindi katika michuano hiyo.

Dkt. Muyungi amesema hana wasiwasi na uimara wa kikosi hicho akiamini kitaendeleza makali ambayo waliyaonesha katika Ligi ya Muungano ya Netiboli yaliyofanyika Zanzibar mapema mwaka huu ambapo timu hiyo ilipoteza mchezo mmoja pekee dhidi ya KVZ na kushinda michezo 10.

Kikosi hicho mara baada ya kutua mkoani Njombe kitaanza mazoezi mepesi tayari kwa ajili ya mawindo ya kubeba ubingwa wa michuano hiyo inaanza Jumatatu ya Aprili 13,2026.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi