Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu Rasmi ya Ofisi ya Makamu wa Rais

Kampeni ya ‘27 ya Kijani, Mti wa Mama’ yatengeneza Fursa Mkoa wa Njombe
Apr 27, 2026
Kampeni ya ‘27 ya Kijani, Mti wa Mama’ yatengeneza Fursa Mkoa wa Njombe
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Anthony Mtaka akiongoza zoezi la wanamichezo wanaoshiriki Mashindano ya Michezo ya Mei Mosi kushiriki zoezi la upandaji miti kupitia Kampeni ya ‘27 ya kijani, Mti wa Mama’ na kufanyika Ofisi za Makao ya Mkoa huo. Pichani Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe Dkt. Stephen Nindi akipanda mti katika eneo hilo≥
Na robert Hokororo

Wanamichezo wanaoshiriki Mashindano ya Michezo ya Mei Mosi wakishiriki zoezi la upandaji miti kupitia Kampeni ya ‘27 ya kijani, Mti wa Mama’ na kufanyika Ofisi za Makao ya Mkoa huo.

Wanamichezo kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais wanaoshiriki Mashindano ya Michezo ya Mei Mosi wakishiriki zoezi la upandaji miti kupitia Kampeni ya ‘27 ya kijani, Mti wa Mama’ na kufanyika Ofisi za Makao ya Mkoa huo.

Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Anthony Mtaka akiwa na Wanamichezo kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais wanaoshiriki Mashindano ya Michezo ya Mei Mosi mara baada ya zoezi la upandaji miti kupitia Kampeni ya ‘27 ya kijani, Mti wa Mama’ na kufanyika Ofisi za Makao ya Mkoa huo.

Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na Wanamichezo wanaoshiriki Mashindano ya Michezo ya Mei Mosi wakishiriki zoezi la upandaji miti kupitia Kampeni ya ‘27 ya kijani, Mti wa Mama’ na kufanyika Ofisi za Makao ya Mkoa huo.

Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Anthony Mtaka akiwa na Wanamichezo kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais wanaoshiriki Mashindano ya Michezo ya Mei Mosi mara baada ya zoezi la upandaji miti kupitia Kampeni ya ‘27 ya kijani, Mti wa Mama’ na kufanyika Ofisi za Makao ya Mkoa huo.

===============================================================================================================

Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Antony Mtaka amesema kampeni ya ‘27 ya Kijani, Mti wa Mama’ imefungua milango ya fursa kwa kaya mbalimbali kubuni miradi ya kibiashara kupitia mazao ya miti.

Mhe. Mtaka amesema hayo Aprili 27, 2026 wakati aliwaongoza wanamichezo wanaoshiriki Mashindano ya Michezo ya Mei Mosi kushiriki zoezi la upandaji miti kupitia Kampeni ya ‘27 ya kijani, Mti wa Mama’ na kufanyika Ofisi za Makao ya Mkoa huo.

Amesema katika Mkoa wa Njombe, kampeni hiyo imewezesha wafanyabiashara, wajasiriamali na kaya mbalimbali kubuni na kuibua fursa za miradi ya kibiashara kupitia miti *na* hivyo kuweza kujiongezea kipato.

“Kihistoria Mkoa wa Njombe umepiga hatua kubwa katika suala la upandaji miti na hivyo Kampeni ya 27 ya Kijani, Mti wa Mama imeendelea kuleta msukumo mkubwa zaidi kwa kaya kuhamasika kupanda miti ya matunda hususani zao la parachichi” amesema Mhe. Mtaka.

Akitolea mfano, Mhe. Mtaka amesema katika halmashauri ya Mji Makambako na Wilaya ya Makete, kila Kaya iliyopo katika Mpango wa TASAF imepatiwa miche 10 ya zao la parachichi na kuipanda ambapo katika kipindi cha miaka mitatu ijayo zao hilo litaanza kuvunwa.

Amesema miche hiyo ya zao la parachichi licha ya kuzalisha matunda pia italeta faida ya kivuli na hivyo kuwahimiza wafanyabiashara na wawekezaji kufika Mkoani humo kwa ajili ya kubaini fursa zilizopo.

Aidha amesema kampeni ya ‘27 ya kijani, Mti wa Mama’ imekusudia kuleta mapinduzi na mageuzi ya kimkakati katika zoezi la upandaji miti nchini kupitia malengo yaliyowekwa na Serikali ya kupanda miti Milioni 10 kila mwaka.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Michezo ya Mei Mosi, Roselyn Massam amesema kamati hiyo na wanamichezo itaendelea kuunga mkono kwa vitendo juhudi za Serikali katika masuala ya Uhifadhi wa Mazingira ikiwemo kushiriki zoezi la upandaji miti.

Tumeshiriki kwa wingi katika zoezi hili ili kuonesha msisitizo wa wanamichezo kuhusu utunzaji wa Mazingira ili kutekeleza maelekezo ya Mhe Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika upandaji wa miti” amesema Bi. Massam. 
 
Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi