







=========================================================================================================
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Richard Muyungi amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) waliotembelea Ofisi ya Makamu wa Rais kwa lengo la kuimarisha ushirikiano katika masuala ya Uhifadhi na Utunzaji wa Mazingira hususan eneo la Mabadiliko ya Tabianchi.
Mazungumzo hayo yamefanyika jijini Dodoma, Aprili 9, 2026 huku Dkt. Muyungi akiwa ameambatana na Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais, Balozi Baraka Luvanda pamoja na Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Mabadiliko ya Tabianchi na Tathmini ya Mazingira,Dkt. Kaniziro Manyika.
Upande wa TADB, Ujumbe wa TADB uliongozwa na Mkurugenzi wa Mipango, Ushauri na masuala ya ushirika Bw. Mkami Waziri aliyeambatana na Afisa Mwandamizi Mipango na Mabadiliko ya Tabianchi Bi. Hawabai Abdulla. Ujumbe huo ulimweleza Katibu Mkuu kuwa masuala ya mabadiliko ya tabianchi yanamgusa kila mmoja. Hali hiyo imepelekea Benki ya TADB kuwa washirika wakubwa katika masuala ya Mazingira na Mabadiliko ya tabianchi.