Maafisa Habari, Mawasiliano, Uhusiano na Itifaki Serikalini wakipandaji miti katika eneo la chanzo cha maji cha Lunyanywi, mjini Njombe, ikiwa ni sehemu ya shughuli za kijamii zinazoambatana na Kikao Kazi cha 21 cha kada hiyo kinachoendelea mkoani Njombe.

===================================================================================================================
Maafisa Habari, Mawasiliano, Uhusiano na Itifaki Serikalini wameungana katika zoezi la upandaji miti katika eneo la chanzo cha maji cha Lunyanywi, mjini Njombe, ikiwa ni sehemu ya shughuli za kijamii zinazoambatana na Kikao Kazi cha 21 cha kada hiyo kinachoendelea mkoani Njombe.
Zoezi hilo limefanyika Mei 8, 2026, likiwa na lengo la kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, za kuhamasisha utunzaji wa mazingira, uhifadhi wa vyanzo vya maji na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi kwa ajili ya maendeleo endelevu ya Taifa.
Akizungumza mara baada ya zoezi hilo, Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO, Kelvin Kanje, amesema Maafisa Habari wana wajibu mkubwa wa kuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira na kuhifadhi vyanzo vya maji kwa manufaa ya Taifa na vizazi vijavyo.
“Kupanda miti ni hatua muhimu katika kulinda mazingira yetu na kuhakikisha vyanzo vya maji vinaendelea kuwepo. Sisi kama Maafisa Habari tunapaswa kuwa mfano kwa jamii kwa kushiriki moja kwa moja shughuli kama hizi zinazogusa maendeleo endelevu ya nchi yetu,” amesema Kanje.
Ameongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kusisitiza utunzaji wa mazingira kama sehemu ya ajenda ya maendeleo, hivyo ni wajibu wa kila Mtanzania kushiriki kikamilifu katika juhudi hizo.
Kwa upande wao, baadhi ya washiriki wa kikao kazi hicho wamesema ushiriki wao katika zoezi hilo unaonesha dhamira ya kada hiyo kuendelea kuhamasisha jamii juu ya umuhimu wa utunzaji wa mazingira kupitia taarifa na kampeni mbalimbali za mawasiliano ya umma.
Agrey Singo ambaye ni Afisa Habari Wizara ya Madini, amesema ushiriki wa maafisa hao katika shughuli za upandaji miti unaonesha mfano wa vitendo katika kuunga mkono ajenda ya kitaifa ya uhifadhi wa mazingira na vyanzo vya maji.
Washiriki wa kikao kazi hicho walipanda miti ya aina mbalimbali inayofaa kwa uhifadhi wa mazingira na vyanzo vya maji, huku wakitoa wito kwa wananchi kuendelea kushiriki katika kampeni za upandaji miti ili kuongeza uoto wa asili na kulinda mazingira kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.
Kikao Kazi cha 21 cha Maafisa Habari, Mawasiliano, Uhusiano na Itifaki Serikalini kimewakutanisha maafisa kutoka taasisi mbalimbali za Serikali kujadili masuala ya mawasiliano ya Serikali, utoaji wa taarifa kwa umma pamoja na mbinu bora za kuimarisha mahusiano kati ya Serikali na wananchi.