Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu Rasmi ya Ofisi ya Makamu wa Rais

Makamu wa Rais akiwasili kumwakilisha Rais Samia Mkutano wa Mabunge ya Maziwa Makuu
Nov 02, 2026
Makamu wa Rais akiwasili kumwakilisha Rais Samia Mkutano wa Mabunge ya Maziwa Makuu
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi akisalimiana na Spika wa Bunge Mhe. Mussa Zungua alipowasili Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa wa Wanawake wa Jukwaa la Mabunge la Ukanda wa Maziwa Makuu (ICGLR), leo Novemba 02, 2026.
Na Robert Hokororo

Makamu wa Rais amewasili katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam kumwakilisha Rais Samia Mkutano wa Mabunge ya Maziwa Makuu.

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa wa Wanawake wa Jukwaa la Mabunge la Ukanda wa Maziwa Makuu (ICGLR).

 

Mkutano huo muhimu pamoja na ajenda nyingine, ni kielelezo cha jitihada kubwa zinazofanywa kuwainua wanawake na nafasi yao muhimu katika kuimarisha uongozi, kudumisha amani na kuchochea maendeleo endelevu. 

 

Pia, ni kudhihirisha dhamira ya kuendeleza misingi ya mshikamano, usawa na ushirikiano wa Kiafrika, ambayo imekuwa sehemu muhimu ya historia ya Bara la Afrika.

 

Historia ya jukwaa hilo inakumbusha nafasi ya kipekee ya Tanzania katika kuhimiza mshikamano na ushirikiano wa kikanda.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi

slot gacor