Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu Rasmi ya Ofisi ya Makamu wa Rais

Makamu wa Rais amwakilisha Rais Dkt. Samia Mkutano wa Wakuu wa Nchi SADC
Dec 17, 2025
Makamu wa Rais amwakilisha Rais Dkt. Samia Mkutano wa Wakuu wa Nchi SADC
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akishiriki katika Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika kwa njia ya mtandao.
Na Robert Hokororo

=======================================================================================

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika kwa njia ya mtandao.

 

Mkutano huo umeongozwa na Mwenyekiti wa mpito wa SADC ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mhe. Cyril Ramaphosa.

 

Aidha, Mkutano huo umepitisha mapendekezo mbalimbali ikiwa ni juhudi ya kuimarisha hali ya amani na usalama katika Jamhuri ya Madagascar na kutoa wito wa mazungumzo ya kitaifa yatakayopelekea uchaguzi huru wa kidemokrasia nchini humo.

 

Halikadhalika, Mkutano huo umeipitisha Jamhuri ya Zambia kuwa Mwenyekiti Ajaye wa Mpito wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

 

Katika Mkutano huo, Makamu wa Rais ameambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Ngwaru Maghembe pamoja na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Said Shaib Mussa.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi