
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni alipowasili Ofisi za Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Makao Makuu Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya ziara ya kikazi leo Julai 2, 2026.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akisalimiana na Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Richard Muyungi alipowasili Ofisi za Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Makao Makuu Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya ziara ya kikazi leo Julai 2, 2026.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akiwasili Makao Makuu ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi Mazingira (NEMC) Mikocheni Jijini Dar es Salaam wakati alipofanya ziara katika Baraza hilo leo tarehe 02 Julai 2026.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akiwasili Makao Makuu ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi Mazingira (NEMC) Mikocheni Jijini Dar es Salaam wakati alipofanya ziara katika Baraza hilo leo tarehe 02 Julai 2026.




Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akizungumza na Viongozi na Watumishi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi Mazingira (NEMC) wakati alipofanya ziara Makao Makuu ya NEMC, Mikocheni Jijini Dar es Salaam leo tarehe 02 Julai 2026.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akikabidhiwa zawadi na Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Dkt. Emmaculate Sware mara baada ya kuzungumza na Viongozi na Watumishi wa Baraza hilo, alipofanya ziara Makao Makuu ya NEMC, Mikocheni Jijini Dar es Salaam leo tarehe 02 Julai 2026.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akikabidhiwa zawadi na Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Dkt. Emmaculate Sware mara baada ya kuzungumza na Viongozi na Watumishi wa Baraza hilo, alipofanya ziara Makao Makuu ya NEMC, Mikocheni Jijini Dar es Salaam leo tarehe 02 Julai 2026.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Dkt. Emmaculate Sware pamoja na Watumishi waliofanya kazi pamoja na Makamu wa Rais wakati akifanya kazi Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC). Picha hiyo imepigwa mara baada ya Makamu wa Rais kukamilisha ziara aliyoifanya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Mikocheni Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 02 Julai 2026.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauniakizungumza wakati wa ziara ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi alipotembelea Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Makao Makuu Jijini Dar es Salaam, Julai 2, 2026.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Richard Muyungi akizungumza wakati wa ziara ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi katika Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Makao Makuu Jijini Dar es Salaam, Julai 2, 2026
.==========================================================================================
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amewasihi watumishi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), kufanya kazi kwa bidii, weledi, ushirikiano na kujiepusha na vitendo vya rushwa ili kuifanya Taasisi hiyo kuwa chachu ya uhifadhi wa mazingira na maendeleo ya Taifa.
Makamu wa Rais ametoa wito huo, alipofanya ziara Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Makao Makuu, Mikocheni Jijini Dar es Salaam. Amewataka watumishi kufanya kazi kwa uadilifu na kutokuwa kikwazo katika utekelezaji wa miradi mikubwa kwa kutanguliza maslahi ya Taifa mbele.
Makamu wa Rais ameipongeza NEMC kwa kutimiza miaka 40 tangu kuanzishwa kwake na kuendelea kuwa chombo kinachohitajika na kutumainiwa nchini.
Aidha, Makamu wa Rais ameipongeza NEMC kwa Mpango Mkakati wa miaka Mitano ambao umeanisha vitu mbalimbali vitakavyowezesha usimamizi na utunzanji wa mazingira kwa ufanisi. Amesema uanzishwaji wa mashindano ya uhifadhi wa mazingira ni muhimu kwa kuwa itakua hamasa ya upandaji miti na usafi kitaifa.
Vilevile, Makamu wa Rais amesema ili kudhibiti masuala ya uchafu ni vema pia kuwatambua wanaokuwa wamefanya vibaya katika mashindano ya usafi na kuwataja hadharani ikiwemo kupatiwa vyeti. Ameiagiza Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, kushirikiana na NEMC katika kufanikisha mashindano ya usafi na utunzaji mazingira nchini.
Halikadhalika Makamu wa Rais, ameitaka NEMC kutilia mkazo suala la nishati safi, matumizi ya teknolojia za kisasa katika kulinda mazingira pamoja na kusimamia vema suala la urejerezaji taka.
Makamu wa Rais, amewapongeza Viongozi wa NEMC kwa kuendelea na mchakato wa kuifanya NEMC kuwa Mamlaka kamili. Amesema suala hilo linashughulikiwa na katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Sita limepewa umuhimu wa kipekee.
Kwa upande wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni amesema suala zima la sekta ya mazingira linaonekana kama la kisheria zaidi lakini mazingira ni zaidi ya sheria kwa kuwa linagusa maeneo mengi.
Pia Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Richard Muyungi amesema katika utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 Ofisi ya Makamu wa Rais imejiwekea msisitizo mambo kadhaa ikiwemo kujenga uchumi wenye ustahilimivu dhidi ya mabadiliko ya tabianchi, kuimarisha hifadhi ya bionuai, misitu, vyanzo vya maji, na mifumo ya ikolojia kama msingi imara wa uchumi katika sekta zote.
Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Dkt. Emmaculate Sware amesema NEMC imeaandaa Mpango Mkakati wa miaka mitano yaani mwaka 2026/2027 – 2030/2031 ambao umelenga kuongeza ufanisi wa usimamizi wa mazingira, kuimarisha matumizi ya teknolojia za kidijitali, kuimarisha ukaguzi na utekelezaji wa sheria pamoja na kuchochea uchumi wa kijani na ustahimilivu wa mabadiliko ya tabianchi.
Ziara hiyo imehudhuriwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Hamad Masauni pamoja na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Richard Muyungi.