Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu Rasmi ya Ofisi ya Makamu wa Rais

Makamu wa Rais atembelea Hospitali ya Mount Meru Arusha
Sep 29, 2026
Makamu wa Rais atembelea Hospitali ya Mount Meru Arusha
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi akiwajulia hali watu mbalimbali wanaopata huduma katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mount Meru, wakati alipofanya kwa ziara ya kustukiza, kukagua huduma mbalimbali Hospitalini hapo. Tarehe 28 Septemba.
Na Robert Hokororo

=============================================================================================

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Deogratius Ndejembi, ametembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Arusha, Mount Meru, kujionea hali ya utoaji wa huduma za afya kwa wananchi pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili wagonjwa na watumishi wa hospitali hiyo.

Mara baada ya kuwasili hospitalini hapo, Makamu wa Rais amepokelewa na viongozi pamoja na watumishi wa hospitali, ambapo taarifa fupi ilitolewa kuhusu maendeleo, utendaji na huduma zinazotolewa, kabla ya kutembelea wodi mbalimbali na kuzungumza na wananchi wanaopata huduma hospitalini hapo.

Akizungumza na wananchi waliolazwa hospitalini hapo, Mhe. Ndejembi aliwapa pole kutokana na maradhi yanayowakabili na kuwafikishia salamu za Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, huku akiwahakikishia kuwa Serikali itaendelea kuipa sekta ya afya kipaumbele na kuboresha huduma zinazotolewa katika vituo vya afya nchini.

Akiwa katika Wodi ya wazazi, Makamu wa Rais alieleza kufurahishwa kuwaona akina mama waliojifungua salama pamoja na watoto wao wakiwa na afya nzuri, akibainisha kuwa Serikali itaendelea kuimarisha huduma za afya ya mama na mtoto ikiwa ni sehemu ya juhudi za kupunguza vifo vinavyotokana na uzazi pamoja na vifo vya watoto.

Alisema jitihada hizo zinaendana na dhamira ya Rais Samia ya kuhakikisha huduma bora na salama za afya ya uzazi zinawafikia wanawake na watoto katika maeneo mbalimbali nchini, sambamba na nafasi yake katika kusukuma mbele ajenda ya kupunguza vifo vya mama na mtoto barani Afrika.

Katika ziara hiyo, Makamu wa Rais pia alipata fursa ya kuzungumza ana kwa ana na baadhi ya wagonjwa kuhusu huduma zinazotolewa hospitalini hapo.

Wagonjwa hao walieleza kuridhishwa na huduma wanazopatiwa, huku baadhi yao wakitaja kushindwa kulipa gharama za matibabu. Kufuatia changamoto hiyo, Makamu wa Rais aliwezesha kulipwa kwa gharama za matibabu za baadhi ya wagonjwa waliokuwa wamekwama kutokana na kutokuwa na uwezo wa kulipa, hatua iliyowapa unafuu wagonjwa hao pamoja na familia zao.

Ziara hiyo imempa Makamu wa Rais nafasi ya kujionea moja kwa moja huduma zinazotolewa katika Hospitali ya Mount Meru, kusikiliza wananchi wanaozitumia na kufahamu changamoto zinazowakabili, huku akisisitiza kuendelea na hatua za kuboresha upatikanaji na ubora wa huduma za afya nchini.

Katika hatua nyingine, Makamu wa Rais alitembelea maeneo mbalimbali ya Jiji la Arusha, kuwasalimu wananchi na kujionea hali ya mazingira mkoani humo.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi

slot gacor