Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu Rasmi ya Ofisi ya Makamu wa Rais

Makamu wa Rais awasili Marekani kushiriki Mkutano wa UNGA81
Sep 22, 2026
Makamu wa Rais awasili Marekani kushiriki Mkutano wa UNGA81
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi akiwa na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Balozi Elsie Kanza, wakati akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa John F Kennedy Jijini New York, kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa 81 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA81). Tarehe 22 Septemba 2026.
Na Robert Hokororo

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi akiwa na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Balozi Elsie Kanza, wakati akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa John F Kennedy Jijini New York, kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa 81 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA81). Tarehe 22 Septemba 2026.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi akisalimiana na Mwakilishi wa Kudumu wa Umoja wa Mataifa – New York Mhe. Balozi Togolani Mavura, wakati akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa John F Kennedy Jijini New York, kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa 81 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA81). Tarehe 22 Septemba 2026.

====================================================================================================================

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi amewasili New York nchini Marekani, ambapo anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa 81 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA81) Unaofanyika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa Jijini New York.

 

Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa John F Kennedy, Makamu wa Rais amepokelewa na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe Balozi Elsie Kanza, Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa – New York Mhe. Balozi Togolani Mavura pamoja na maafisa mbalimbali.

 

Kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kinachoshirikisha Wakuu wa Nchi na Viongozi mbalimbali ni Mkutano muhimu ambao, pamoja na mambo mengine, hujadili masuala ya kiuchumi, kisiasa, mazingira na haki za binadamu. 

Kikao hicho kinafanyika chini ya Kaulimbiu isemayo "Kurudisha Imani, Kusimamia Mabadiliko, Umoja wa Mataifa unaohudumia wote” (Restoring Trust, Managing Transformation: A United Nations That Delivers for All). Kaulimbiu hiyo ni wito wa pamoja wa kujenga upya uaminifu na ushirikiano wa kimataifa pamoja na kusimamia vema mabadiliko makubwa yanayoendelea ulimwenguni ikiwemo kasi ya ukuaji wa akili unde (AI).

Aidha, Mheshimiwa Makamu wa Rais anatarajiwa kuhutubia Kikao cha 81 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa pamoja na kushiriki kwenye vikao mbalimbali ikiwemo Mjadala Mkuu (General Debate), Mikutano ya pembezoni na Mikutano ya pande mbili (Bilateral Meetings)

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi

slot gacor