Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu Rasmi ya Ofisi ya Makamu wa Rais

Mhandisi Masauni amzungumzia Hayati Sheikh Karume
Apr 07, 2026
Mhandisi Masauni amzungumzia Hayati Sheikh Karume
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni amesema Hayati Sheikh Abeid Amani Karume akizungumza mara baada ya kushiriki Dua maalum ya kumuombea kiongozi huyo ikiwa ni miaka 54 ya kifo chake iliyofanyika Afisi Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kisiwandui Unguja, Aprili 7, 2026.
Na Robert Hokororo

=============================================================================================================

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni amesema Hayati Sheikh Abeid Amani Karume alikuwa mtu ambaye anapenda umoja, ushirikiano na muumini wa muungano.

Amesema matendo ya Hayati Karume yanadhihirisha hasa wakati wa ukombozi namna alivyopambana na wakoloni ambao hawakutaka kuiachia Zanzibar na ndio muasisi wa Muungano wetu na alikuwa mstari wa mbele wakati Tanzania ikishirikishiriana na mataifa mengine ambayo yalikua hayajapata uhuru

Mhe. Masauni anasema, Karume alikuwa mtu asiyependa uonevu, alikua mtetezi wa watu wa chini, hakupenda unyonyaji na alileta mapinduzi makubwa kwa kutoa ardhi kwa wahitaji, alianzisha sera ya elimu bure, afya bure na makazi bora kwa wananchi.

Ameongeza kuwa kiongozi huyo alikua akiwaangalia zaidi watu wa hali ya chini, hivyo kuna kila sababu ya kumuenzi kwa mambo mengi yasiyoelezeka kwa kuacha msingi mikubwa na imara katika kubadilisha Maisha ya watu.

Mhe. Masauni ameyasema hayo aliposhiriki Dua maalum ya kumuombea kiongozi huyo ikiwa ni miaka 54 ya kifo chake iliyofanyika Afisi Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kisiwandui Unguja, Aprili 7, 2026.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi