Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu Rasmi ya Ofisi ya Makamu wa Rais

Naibu Waziri Kwagilwa atoa saa 24 kusafisha mfereji geita
Sep 22, 2026
Naibu Waziri Kwagilwa atoa saa 24 kusafisha mfereji geita
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Reuben Kwagilwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Alexander Mnyeti alipowasili mkoani humo kwa jailli ya ziara ya kikazi.
Na Robert Hokororo

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Reuben Kwagilwa akizungumza wakati wa ziara ya kikazi mkoani Geita.

==================================================================================================================

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Reuben Kwagilwa ametoa saa 24 kwa Halmashauri ya Manispaa ya Geita kuanza kusafisha mfereji wa maji ya mvua unaotajwa kusababisha mafuriko katika eneo la Mbugani.

Kwagilwa ametoa agizo hilo akita katika ziara ya kikazi mkoani Geita kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni baada ya kupewa taarifa kuwa zoezi la usafi limekwama kutokana na kuharibika kwa mitambo ya Halmashauri.

Ameagiza mitambo ikodishwe haraka kwa kuwa msimu wa mvua umekaribia na kunatarajiwa mvua kubwa za El Niño.

 

“Hiki ninachokielekeza nina uhakika kitafanyika na lazima kuwezekane kufanyika, hamuwezi mkawa mnakusanya bilioni 17 halafu kwenye hiyo bilioni 17 hamuoni kuwa hili ni tatizo la kushughulikia, kesho hapa pafanyiwe usafi,” amesema Mhe. Kwagilwa.

Halmashauri hiyo hukusanya takribani Sh bilioni 17 kwa mapato ya ndani kwa mwaka,hivyo ameelekeza sehemu ya mapato hayo itumike kushughulikia changamoto zinazoweza kuhatarisha wananchi wanaoishi na wanaopita katika eneo hilo la barabara ya Geita–Katoro.

Awali, baadhi ya wananchi walitoa maoni na kupendekeza hatua mbadala za kukabiliana na changamoto ya mafuriko kabla ya mvua kuanza, huku Mhe. Kwagilwa akitaka Halmashauri kuchukua hatua za haraka ili kuzuia madhara yanayoweza kujitokeza.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi

slot gacor