Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu Rasmi ya Ofisi ya Makamu wa Rais

Ofisi ya Makamu wa Rais kuendeleza Michezo kwa Watumishi
May 08, 2026
Ofisi ya Makamu wa Rais kuendeleza Michezo kwa Watumishi
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Richard Muyungi akitembelea na kukagua eneo litakalojengwa uwanja wa michezo wa Ofisi ya Makamu wa Rais lililopo Ipala jijini Dodoma leo Mei 08, 2026.
Na Robert Hokororo

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Richard Muyungi amesema Ofisi hiyo itaendelea kuimarisha na kuendeleza michezo kwa watumishi ili kuwajenga kiafya.

Amesema hayo alipotembelea na kukagua eneo litakalojengwa uwanja wa michezo wa Ofisi ya Makamu wa Rais lililopo Ipala jijini Dodoma leo Mei 08, 2026.

Dkt. Muyungi alisema kuwa uwanja huo ukikamilika utatoa fursa kwa taasisi zingine kupata maeneo ya michezo.

Aliongeza kuwa uwanja huo utakapokamilika utakuwa ni chachu kwa watumishi wa Ofisi hiyo kuimarisha ushirikiano na taasisi zingine kupitia michezo.

“Kama tunavyofahamu michezo si tu burudani bali ni sehemu ya kulinda afya zetu kupitia mazoezi mbalimbali ya viungo,” alisema.

Katika ziara hiyo Dkt. Muyungi aliambatana na Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Balozi Baraka Luvanda na Menejimenti ya Ofisi hiyo.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi

slot gacor