
Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Kemilembe Mutasa akifanya mazungumzo na Mkuu wa Masuala ya Maji na Usafi wa Mazingira wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF Tanzania)Bi. Gemma Querol aliyeambatana na Meneja wa Masuala ya Maji na Usafi wa Mazingira Mhandisi Stanislaus Kamwaga.

Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Kemilembe Mutasa akiagana na Mkuu wa Masuala ya Maji na Usafi wa MazingiraShirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF Tanzania) Bi. Gemma Querol mara baada ya kufanya mazungumzo katika Ofisi ya Makamu wa Rais iliyopo Mji wa Serikali, Mtumba jijini Dodoma leo Mei 08, 2026.

Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Kemilembe Mutasa (wa pili kulia mbele) akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Masuala ya Maji na Usafi wa Mazingira Bi. Gemma Querol aliyeambatana na Meneja wa Masuala ya Maji na Usafi wa Mazingira Mhandisi Stanislaus Kamwaga mara baada ya kikao na wataalamu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais zilizopo katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma Mei 08, 2026.
=================================================================================================================
Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF Tanzania) zinatarajia kushirikiana katika utekelezaji wa malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Hayo yamejiri wakati wa kikao kati ya Ofisi ya Makamu wa Rais na Ujumbe kutoka UNICEF Tanzania kilichofanyika katika Ofisi ya Makamu wa Rais iliyopo Mji wa Serikali, Mtumba jijini Dodoma leo Mei 08, 2026.
Katika kikao hicho Mkurugenzi wa Mazingira Bi. Kemilembe Mutasa amefanya mazungumzo na Mkuu wa Masuala ya Maji na Usafi wa Mazingira wa UNICEF Tanzania Bi. Gemma Querol aliyeambatana na Meneja wa Masuala ya Maji na Usafi wa Mazingira Mhandisi Stanislaus Kamwaga.
Katika mazungumzo yao watendaji hao wamejadili kuhusu utekelezaji wa sera na mikakati muhimu iliyopo katika kufikia malengo ya utekelezaji wa nguzo ya tatu Dira hiyo inayozungumzia Uhifadhi wa Mazingira na Ustahimilivu dhidi ya Mabadiliko ya Tabianchi.
Kikao hicho kiliwashirikisha pia Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Mabadiliko ya Tabianchi na Tathmini kwa Mazingira Dkt. Kanizio Manyika, Mkurugenzi Msaidizi – Sehemu ya Udhibiti na Uchafuzi wa Mazingira Bw. Thomas Chali pamoja na Wataalamu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais.