

Mkurugenzi wa Muungano Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Juma Mohamed Salum akifungua Kikao Kazi cha kuwajengea uwezo Watu wenye ushawishi (Digital Influencers) kuhusu Mpango Mkakati wa Elimu kwa Umma kuhusu Muungano kupitia mitandao ya Jamii kilichofanyika Septemba 29,2026 katika ukumbi wa FCC, Dar Es Salaam.











Ofisi ya Makamu wa Rais imefanya kikao kazi cha kuwajengea uwezo Watu wenye ushawishi (Digital Influencers) kuhusu Mpango Mkakati wa Elimu kwa Umma kuhusu Muungano kupitia mitandao ya Jamii.
Wakati wa Kikao kazi hicho, Mada mbalimbali kuhusu Hiatoria, fursa ,faida na Mafanikio ya Muungano ziliwasilishwa na Wataalam kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais pamoja na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais.
Aidha Maswali yanayoulizwa mara kwa mara, Umuhimu wa Elimu kwa Umma kuhusu Muungano pamoja na Mbinu za Utoaji wa Elimu Kuhusu Muungano ziliwasilishwa na kujadiliwa kwa kina.
‘Digital Influencers’ wapatao 30
kutoka maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na vijana kutoka Taasisi ya Uzalendo na Vijana Tanzania (TAUVITA), wameahidi kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Rais katika kuelimisha Umma kuhusiana na masuala ya Muungano.
Kikao kazi hicho kilifunguliwa na kufungwa na Dkt. Juma Salum, Mkurugenzi wa Muungano Ofisi ya Makamu wa Rais, Septemba 29,2026 katika ukumbi wa FCC, Dar Es Salaam.