
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (kulia) akizungumza na Naibu Waziri wa Malisili na Utalii Mhe. Hamad Hassan Chande wakati wa Kikao cha Saba cha Mkutano wa Tatu Bunge la 13 jijini Dodoma leo Aprili 13, 2026. Mbele ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Prof. Riziki Shemdoe.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (kulia) akizungumza na Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Salome Makamba wakati wa Kikao cha Saba cha Mkutano wa Tatu Bunge la 13 jijini Dodoma leo Aprili 13, 2026.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (kulia) akizungumza na Naibu Waziri wa Malisili na Utalii Mhe. Hamad Hassan Chande wakati wa Kikao cha Saba cha Mkutano wa Tatu Bunge la 13 jijini Dodoma leo Aprili 13, 2026. Mbele kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Prof. Riziki Shemdoe na Naibu Waziri wa TAMISEMI Mhe. Dkt. Festo Dugange.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Reuben Kwagilwa (kulia) akizungumza na Mbunge wa Nachingwea Mhe. Fadhili Liwaka wakati wa Kikao cha Saba cha Mkutano wa Tatu Bunge la 13 jijini Dodoma leo Aprili 13, 2026. Aliyekaa mbele ni Naibu Waziri wa Madini Mhe. Dkt. Steven Kiruswa.


Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Reuben Kwagilwa (kulia) akizungumza na Mbunge wa Nachingwea Mhe. Fadhili Liwaka wakati wa Kikao cha Saba cha Mkutano wa Tatu Bunge la 13 jijini Dodoma leo Aprili 13, 2026. Kushoto ni Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Mhandisi Mshamu Munde na aliyekaa mbele ni Naibu Waziri wa Madini Mhe. Dkt. Steven Kiruswa.

Mbunge wa Jimbo la Tanganyika Mhe. Moshi Kakoso akichangia Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2026/27 bungeni jijini Dodoma leo Aprili 13, 2026.
========================================================================================
Serikali imeombwa kuongeza mikakati kufanikisha biashara ya kaboni inakuwa endelevu na kunufaisha wananchi hususan wale wanaozungukwa na misitu.
Wito huo umetolewa na Mbunge wa Jimbo la Tanganyika Mhe. Moshi Kakoso wakati akichangia Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2026/27 bungeni jijini Dodoma leo Aprili 13, 2026.
Katika mchango wake Mhe. Kakoso alisema ipo misitu mingi nchini ambayo endapo mikakati itawekwa katika usimamizi wa biashara ya kaboni, itafanikisha kuwa na miradi ambayo itaingizia Serikali mapato.
Hivyo, aliomba Serikali kuweka mazingira wezeshi kwa jamii hasa kwenye maeneo ambayo yana misitu ikiwemo Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi ili wananchi wanufaike na biashara ya kaboni.
Katika kuimarisha usimamizi wa biashara hiyo, tayari Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais imeanzisha Kituo cha Taifa cha Kuratibu Kaboni (NCMC) ambacho ambacho kinaendelea kusajili miradi ya kaboni na kuelimisha wananchi kuhusu namna ya kutunza misitu ili kunufaika na biashara hiyo.
Serikali inaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wadau wote ili kuhamasisha uwekezaji wa miradi ya biashara ya kaboni kwa wadau mbalimbali ili kuwa na uelewa wa pamoja.
Sanjari na hatua hiyo, Ofisi ya Makamu wa Rais ilitunga Kanuni za mwaka 2022 na marekebisho yake ya mwaka 2023 ambazo zinasimamia baishara ya kaboni nchini.