Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu Rasmi ya Ofisi ya Makamu wa Rais

Serikali yakoleza moto kukabili mabadiliko ya tabianchi
May 07, 2026
Serikali yakoleza moto kukabili mabadiliko ya tabianchi
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mazingira anaeshughulikia masuala ya Mabadiliko ya Tabianchi Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Kanizio Manyika akiongoza kikao kazi na Shirika lisilo la kiserikali linalojishughulisha na uhifadhi na utunzaji wa mazingira la Kazzi Africa Holdings (T) Ltd leo Mei 07, 2026 jijini Dodoma katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Makamu wa Rais Mtumba.
Na Robert Hokororo

Afisa Misitu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Timoteo Mande akitoa neno la utambulisho wakati wa kikao kazi leo Mei 07, 2026 jijini Dodoma katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Makamu wa Rais Mtumba.

Bw. Rumisho Shikonyi kutoka Taasisi ya Kazzi Africa Holdings (T) Ltd. Akifafanua jambo wakati wa kikao kazi leo Mei 07, 2026 jijini Dodoma katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Makamu wa Rais Mtumba.

Washiriki wakiwa katika kikao kazi leo Mei 07, 2026 jijini Dodoma katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Makamu wa Rais Mtumba.

Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kushiriki katika kikao kazi leo Mei 07, 2026 jijini Dodoma katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Makamu wa Rais Mtumba.

===========================================================================================

Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais imeendeleza juhudi zake katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi na kuhakikisha usimamizi wa mazingira unakuwa endelevu.

Hayo yamedhihirika wakati wa kikao cha Wataalamu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais wakiongozwa na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mazingira anaeshughulikia masuala ya Mabadiliko ya tabianchi Dkt.Kanizio Freddy Manyika wamefanya kikao kazi na Shirika lisilo la kiserikali linalojishughulisha na uhifadhi na utunzaji wa mazingira la    Kazzi Africa Holdings (T) Ltd leo Mei 07, 2026 jijini Dodoma katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Makamu wa Rais Mtumba.

Kikao kazi hicho kilichowashirikisha pia wataalamu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI); Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Kituo cha Taifa cha Kuratibu Kaboni (NCMC), Wizara ya Ardhi, Nyumba na Makazi pamoja na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kilicholenga kujadili utekelezaji wa Progamu ya ‘Otesha Afrika’ inayohusu uhamasishaji na upandaji wa miti katika maeneo mbalimbali nchini.

Akifungua kikao hicho, Dkt. Manyika alisema Serikali itaendelea kushirikiana na wadau katika kuhakikisha jukumu la kulinda na kuhifadhi mazingira linakuwa endelevu.

Alieleza kuwa Mabadiliko ya tabianchi ni changamoto ambayo inaweza kugeuka fursa kwa wadau na wananchi kwa ujumla kushiriki katika kampeni za upandaji wa miti.

“Sote tunatambua kuwa kila tarehe 17 ya mwezi Juni tunaadhimisha Siku ya Kupambana na Kuenea kwa Jangwa ambayo kwa namna moja ama nyingine inaweza kuongezewa nguvu na ushiriki wa wadau katika kampeni za upandaji wa miti,” alisema.

Kwa upande wake Bw. Rumisho Shikonyi kutoka Taasisi ya Kazzi Africa Holdings (T) Ltd. aliomba pawepo na nguvu ya pamoja kati ya Serikali na wadau kuhakikisha utamaduni wa upandaji wa miti na kuitunza unakuwa endelevu.

Walisema ili kufanikisha malengo hayo walihimiza uwekezaji wa elimu ya upandaji wa miti hususan kwa kundi la watoto na vijana ambao ni idadi kubwa.

Aidha, washiriki wa kikao hicho wamejadiliana kuhusu usimamizi na ufuatiliaji wa miti inayopandwa na takwimu zake pamoja na ushirikishwa wa wadau katika shughuli za upandaji wa miti.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi

slot gacor