Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu Rasmi ya Ofisi ya Makamu wa Rais

Uchumi wa Buluu kuineemesha Tanzania
Apr 15, 2026
Uchumi wa Buluu kuineemesha Tanzania
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Richard Muyungi (katikati) akishiriki kikao cha Makatibu Wakuu wa Sekta zenye mnasaba na Uchumi wa Buluu kilichofanyika jijini Dodoma leo Aprili 15, 2026.
Na robert Hokororo

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Richard Muyungi (katikati) akishiriki kikao cha Makatibu Wakuu wa Sekta zenye mnasaba na Uchumi wa Buluu kilichofanyika jijini Dodoma leo Aprili 15, 2026. 

Naibu Katibu Mkuu (Elimu) Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Hussein Omar (kulia) akishiriki kikao cha Makatibu Wakuu wa Sekta zenye mnasaba na Uchumi wa Buluu kilichofanyika jijini Dodoma leo Aprili 15, 2026.

Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Uchumi wa Buluu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Magdalena Ngotolainyo (kulia) na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu Dkt. Kanizio Manyika wakishiriki kikao cha Makatibu Wakuu wa Sekta zenye mnasaba na Uchumi wa Buluu kilichofanyika jijini Dodoma leo Aprili 15, 2026.

Wakishiriki wakifuatilia kikao cha Makatibu Wakuu wa Sekta zenye mnasaba na Uchumi wa Buluu kilichofanyika jijini Dodoma leo Aprili 15, 2026.

Wakishiriki wakifuatilia kikao cha Makatibu Wakuu wa Sekta zenye mnasaba na Uchumi wa Buluu kilichofanyika jijini Dodoma leo Aprili 15, 2026.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Richard Muyungi (aliyekaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na washiriki baada ya kufungua kikao cha Makatibu Wakuu wa Sekta zenye mnasaba na Uchumi wa Buluu kilichofanyika jijini Dodoma leo Aprili 15, 2026. 

==========================================================================================

Tanzania inatarajia kunufaika kikamilifu na fursa za Uchumi wa Buluu na kuchangia kwa kiwango kikubwa katika pato la taifa, ajira na ustawi wa wananchi.

 

Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Richard Muyungi wakati akifungua kikao cha Makatibu Wakuu wa Sekta zenye mnasaba na Uchumi wa Buluu uliofanyika jijini Dodoma leo Aprili 15, 2026.

 

Amesema kuwa Mpango wa miaka mitano wa Matumizi ya Maeneo ya Maji (MSP) ni mchakato wakimkakati utakaowezesha taifa kupanga matumizi ya maeneo ya maji kwa kuzingatia mahitaji ya kiuchumi, kijamii na kimazingira. 

 

Aidha, Dkt. Muyungi alieleza kuwa kupitia Mpango huo itasaidia kupunguza migongano ya matumizi ya rasilimali za maji, kuongeza uhakika wa uwekezaji na kuhakikisha uhifadhi na matumizi endelevu ya rasilimali za maji.

 

Aliongeza kuwa Mpango kazi wa utekelezaji wa shughuli za Uchumi wa Buluu

kwa mwaka 2026/27, umeandaliwa kwa lengo la kurahisisha uratibu na utekelezaji wa shughuli za Uchumi wa Buluu nchini ili kufikia malengo mahsusi yaliyoainishwa katika Sera ya Taifa ya Uchumi wa Buluu ya mwaka 2024 na Mkakati wake wa utekelezaji.

 

Awali akimkaribisha mgeni rasmi, Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Balozi Baraka Luvanda alisema kikao hicho ni muhimu kwa ajili ya kupitia hatua zilizofikiwa katika utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uchumi wa Buluu (Julai-Desemba 2025).

 

Balozi Luvanda alieleza kuwa washiriki wanapata nafasi ya kujadili mafanikio, changamoto pamoja na kuweka mikakati madhubuti ya kuboresha utekelezaji wake. 

 

“Kikao hiki kitatupatia fursa ya kupitia na kuridhia Mpango Kazi wa utekelezaji wa shughuli za Uchumi wa Buluu kwa mwaka wa fedha 2026/27, ili khakikisha kuwa sekta zote husika zinaendelea kushirikiana kwa ufanisi katika kukuza mchango wa Uchumi wa Buluu katika maendeleo ya taifa letu,” alisema.

 

Halikadhalika, Balozi Luvanda alisema kupitia kikao hicho washiriki wanajadili Mpango Kazi wa Uandaaji wa Mpango wa Matumizi Endelevu ya Maeneo ya Maji (Marine Spatial Planning -MSP) kwa kipindi cha mwaka 2025-2030, ambao ni nyenzo muhimu katika kupanga na kusimamia matumizi endelevu ya rasilimali za bahari na maji baridi kwa ujumla, kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.

 

Ikumbukwe kuwa Ofisi ya Makamu wa Rais imepewa majukumu la kuratibu utekelezaji wa shughuli za Uchumi wa Buluu Tanzania Bara ikiwemo kuratibu vikao vya Kamati ya Makatibu Wakuu na Kamati ya Mawaziri wa sekta zenye mnasaba na masuala ya Uchumi wa Buluu. 

 

Pia, ina jukumu la kuhakikisha inaratibu, inafuatilia na kufanya tathmini ya utekelezaji wa shughuli za Uchumi wa Buluu nchini, ikiwemo shughuli zinazotekelezwa na sekta zenye mnasaba na masuala ya Uchumi wa

Buluu.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi