Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu Rasmi ya Ofisi ya Makamu wa Rais

Wabunge waaswa kuacha kutumia karatasi kulinda mazingira
Apr 10, 2026
Wabunge waaswa kuacha kutumia karatasi kulinda mazingira
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mussa Azzan Zungu akiongoza cha Kikao cha Bunge leo Aprili 10, 2026.
Na Robert Hokororo

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Reuben Kwagilwa (kulia) akishiriki kikao cha Sita cha Mkutano wa Tatu wa Bunge la 13 jijini Dodoma leo Aprili 09, 2026.

=========================================================================================

Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamehimizwa kupunguza matumizi ya karatasi na kutumia mfumo wa kidijitali katika shughuli za Bunge ili kukabiliana na changamoto ya uchafuzi wa mazingira.

Wito huo umetolewa bungeni jijini Dodoma na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mussa Azzan Zungu wakati akiongoza cha Kikao cha Bunge leo Aprili 10, 2026.

Alisema kuwa mojawapo ya shughuli zinazochangia uchafuzi wa mazingira ni pamoja na matumizi makubwa ya karatasi hivyo kila mtu ana wajibu wa kuhakikisha mazingira yanatunzwa.
“Bado kuna Waheshimiwa Wabunge wanaomba kuchangia kwa kutumia karatasi, hizi karatasi zinachafua mazingira kwenye nchi yetu, kwahiyo niwaombe sana mtumie mfumo huu ni rahisi sana,” alisisitiza Mhe. Zungu.

Aidha, ili kukabiliana na uchafuzi wa mazingira tayari Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais na taasisi mbalimbali imeendelea kuchukua hatua madhubuti zikiwemo kutumia mifumo mbalimbali ya mtandao katika katika utendaji.

Mifumo ya mtandao inawezesha utekelezaji wa shughuli za Serikali zikiwemo za Bunge kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) hivyo kurahisisha utendaji na kupunguza matumizi ya karatasi.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi