
Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Makatibu Tawala wa Mikoa mara baada ya kufungua Kikao cha Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakurugenzi wa Halmashauri kuhusu Programu ya Mageuzi ya Kimkakati ya Mazingira Endelevu Tanzania, kilichofanyika Dodoma, Aprili 16, 2026.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi wa Halmashauri mara baada ya kufungua Kikao cha Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakurugenzi wa Halmashauri kuhusu Programu ya Mageuzi ya Kimkakati ya Mazingira Endelevu Tanzania, kilichofanyika Dodoma, Aprili 16, 2026.

Naibu Katibu Mkuu (Mazingira), Ofisi ya Makamu wa Rais, Balozi Baraka Luvanda akizungumza wakati wa Kikao cha Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakurugenzi wa Halmashauri kuhusu Programu ya Mageuzi ya Kimkakati ya Mazingira Endelevu Tanzania, kilichofanyika Dodoma, Aprili 16, 2026.

Naibu Katibu Mkuu (Muungano), Ofisi ya Makamu wa Rais, Bw. Abdallah Mitawi akishiriki Kikao cha Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakurugenzi wa Halmashauri kuhusu Programu ya Mageuzi ya Kimkakati ya Mazingira Endelevu Tanzania, kilichofanyika Dodoma, Aprili 16, 2026.


Baadhi ya Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakurugenzi wa Halmashauri wakiwa katika Kikao kuhusu Programu ya Mageuzi ya Kimkakati ya Mazingira Endelevu Tanzania, kilichofanyika Dodoma, Aprili 16, 2026.

Baadhi ya watendaji kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais wakiwa katika Kikao kuhusu Programu ya Mageuzi ya Kimkakati ya Mazingira Endelevu Tanzania, kilichofanyika Dodoma, Aprili 16, 2026.

Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Kemilembe Mutasa akizungumza wakati wa Kikao cha Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakurugenzi wa Halmashauri kuhusu Programu ya Mageuzi ya Kimkakati ya Mazi ngira Endelevu Tanzania, kilichofanyika Dodoma, Aprili 16, 2026

Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Menejimenti ya Ofisi ya Makamu wa Rais mara baada ya kufungua Kikao cha Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakurugenzi wa Halmashauri kuhusu Programu ya Mageuzi ya Kimkakati ya Mazingira Endelevu Tanzania, kilichofanyika Dodoma, Aprili 16, 2026.
===============================================================================================
Wananchi wameaswa kuchangamkia fursa zinazopatikana kwenye Biashara ya Kaboni kwa kuanzisha miradi mbalimbali kulingana na jeografia ya eneo husika na kuachana na dhana ya upandaji miti na misitu ndio inakopatikana Biashara ya Kaboni.
Hayo ameyasemwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Richard Muyungi wakati akifungua Kikao cha Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakurugenzi wa Halmashauri kuhusu Programu ya Mageuzi ya Kimkakati ya Mazingira Endelevu Tanzania, kilichofanyika Dodoma, Aprili 16, 2026 akieleza kuwa kuna fursa katika program hiyo ikiwemo Biashara ya Kaboni.
Amesema fursa ya Biashara ya Kaboni haipo pekee kwenye upandaji miti kama ambavyo wengi wanadhani, bali katika Nishati Safi ya Kupikia, Miradi ya Taka, Usafishaji wa Miji, Taka Nngumu na taka zingine zote zinaweza kuwa fursa katika Biashara hiyo.
Baada ya Serikali kuzindua Dira 2050 Ofisi ya Makamu wa Rais imeandaa Programu ya Mageuzi ya Kukijanisha Tanzania kwa kipindi cha mwaka 2026 hadi 2030, inayolenga kuchagiza matokeo makubwa ya kurejesha uoto wa asili, kuimarisha ustawi wa mifumo ikolojia na kuongeza mchango wa rasilimali katika Pato la Taifa, sambamba na kuchangia katika kufikia malengo ya Dira 2050.
“Ili tuwe na mchango mkubwa kwenye Dira 2050 tunatakiwa kuwa na mpango maalum na hatutakuwa tukiangali katika upandaji miti pekee bali tutaangali pia kwenye Nishati safi ya Kupikia ili kuwafikia wananchi.
Ameongeza kuwa kutokana na heshima ambayo mazingira yamepewa na kuwekwa kwenye Dira 2050 ni vyema sekta ya mazingira nayo ibadilike ili mchango wake uonekane kwa kuyasimamia mazingira vizuri.
“Awali, Naibu Katibu Mkuu (Mazingira), Ofisi ya Makamu wa Rais, Balozi Baraka Luvanda alisema Programu hii inalenga kuchagiza matokeo makubwa na ya haraka katika kurejesha uoto wa asili, ustawi wa mifumo ikolojia na kuimarika kwa huduma za kiikolojia ambazo zinachangia katika sekta mbalimbali za uzalishaji nchini.”
“Programu hii itatekelezwa Tanzania bara na Zanzibar kwa kuongeza eneo lenye uoto wa kijani kupitia upandaji miti kwa wingi na usimamizi wa mazingira. Ili kupunguza uharibifu wa ardhi na ardhi-oevu, kurejesha ardhi na misitu iliyoharibiwa na kukijanisha miji yetu.”
“Jitihada hizi zitachangia katika kupunguza utegemezi wa kuni na mkaa; Kurejesha hekta milioni 5 za ardhi, misitu, ardhi-oevu na nyanda za malisho zilizoharibiwa; Kuhamasisha usafi wa mazingira na uchumi rejeshi katika usimamizi wa taka.
Ameongeza kuwa Maeneo ya kimkakati ya utekelezaji wa Programu ya Mageuzi ya kukijanisha Tanzania ni Upandaji Miti katika Mikoa ya Tabora, Mwanza, Shinyanga, Kigoma, Geita, Singida, Simiyu, Manyara, Kilimanjaro, Arusha, Dodoma, Rukwa na Zanzibar.
Shughuli zingine ni pamoja na uanzishwaji wa Bustani za kijani katika maeneo ya miji; Utunzaji na urejeshaji wa maeneo oevu ya Ziwa Natron, Bonde la Mto Mara, Bonde la Mto Malagarasi Myovosi na Bonde la Mto kilombero; kudhibiti viumbe vamizi katika maeneo ya Mikoa ya Dodoma, Arusha, Mara, Mwanza na Manyara; usafi wa mazingira na urejelezaji wa taka ngumu.
Aidha, Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Kemilembe Mutasa alisema katika utekelezaji wake, Programu hii itaweka mkazo katika hatua za kimkakati ikiwemo kukuza uelewa wa umma kuhusu masuala ya hifadhi na usimamizi wa mazingira, kuhamasisha ushiriki wa wadau katika ngazi zote hususan ngazi za Mamlaka za Serikali za Mitaa pamoja na kuweka mfumo madhubuti wa ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa Programu hii muhimu.